Habari za Punde

Wahitimu 30 wa Kidatu Cha Sita Kisiwani Pemba Waliopata Division One Watunikiwa Zawadi.

Waziri  wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe.Riziki Pembe Juma, akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Mhe.Omar Khamis Othaman mara baada ya kuwasili, katika Hoteli ya Pemba Misali Sanset Beach kwa ajili ya kutoa zawadi kwa wanafunzi 30 wa Pemba waliopata daraja la kwanza katika mitihani ya Kidato cha sita mwaka 2018.
MKUU wa Mkoa wa kusini Pemba Hemed Suleiman Abdalla wa kwanza kulia, akimuongoza waziri wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali zanzibar Riziki Pembe Juma, kwenda katika ukumbi kwa ajili ya kutoa zawadi kwa wanafunzi 30 wa Pemba, waliofanya vizuri katika mitihani yao ya kidato cha Sita na Kupata daraja la kwanza 2018
VIONGOZI mbali mbali wa Serikali wakiongozwa na maafisa wa kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa kusini Pemba, wakiimba wimbo maalumu wa Taifa, kabla ya kuanza kwa hafla ya kuwatunuku zawadi wanafunzi 30 wa Pemba waliopata daraja la kwanza Kidato cha sita mwaka 2018, hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Pemba Misali Sanset Beach Wesha Mjini Chake Chake
MKUU wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Omar Khamis Othman akizungumza katika hafla ya kuwatunuku zawadi wanafunzi 30 wa Pemba, waliopata daraja la kwanza kidato cha sita mwaka 2018 hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Pemba Misali Sanset Beach Wesha Mjini Chake Chake
KATIBU Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Dkt Idrisa Muslimu Hijja, akizungumza katika kikao cha kutoa zawadi kwa wanafunzi 30 wa Pemba, waliopata daraja la kwanza kidato cha Sita mwaka 2018,hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Pemba Misali Sanset Beach Wesha Mjini Chake Chake
WAZIRI wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Riziki Pembe Juma, akizungumza katika hafla ya kuwakabidhi zawadi wanafunzi 30 waliopata daraja la kwanza kidato cha sita mwaka 2018, hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Pemba Misali Sanset Beach Wesha Mjini Chake Chake
WAZIRI wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Riziki Pembe Juma, akimkabidhi mmoja ya wanafunzi waliopata daraja la kwanza kidato cha sita mwaka 2018, laptop moja na zawadi mbali mbali zilizotolewa na Green Light kwa kushirikiana na wafanya biashara mbali mbali Zanzibarhafla iliyofanyika katika ukumbi wa Pemba Misali Sanset Beach Wesha Mjini Chake Chake.
VIONGOZI mbali mbali wa Taasisi Binafsi, wafanya biashara na watendaji wa Serikali wakiwa katika hafla ya kukabidhi zawadi kwa wanafunzi 30 wa Kisiwa cha Pemba, waliofanya vizuri katika mitihani yao ya kidato cha sita mwaka 2018 na kupata daraja la kwanza,hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Pemba Misali Sanset Beach Wesha Mjini Chake Chake
VIONGOZI mbali mbali wa Serikali, Vyama vya siasa, walimu, wanafunzi na wazazi wakifuatilia kwa makini zoezi la utoaji wa zawadi kwa wanafunzi 30 wa pemba waliopata daraja la kwanza kidato cha sita mwaka 2018 na kupatiwa zawadi mbali mbali ikiwemo Laptop moja kwa kila mwanafunzi, hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Pemba Misali Sanset Beach Wesha Mjini Chake Chake.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

1 comment:

  1. Picha nyengine za wanafunzi wakikabidhiwa zawadi zipo au...?

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.