Habari za Punde

Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Ashiriki Mazishi ya Wananchi Waliofariki Katika Ajali ya Kivuko cha Mv Nyerere Mwanza leo.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimia na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama  wakati alipowasili katika kijiji cha Bwasa kwenye  kisiwa cha Ukara wilayani Ukerewe kushiriki katika mazishi ya wananchi waliofariki dunia katika ajali ya kivuko cha MV Nyerere, 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Mbunge wa Ilemela, Angelina Mabula na viongozi wengine walioshiriki katika mazishi ya  baadhi ya wananchi waliofariki dunia katika ajali ya meli ya MV Nyerere katika kisiwa cha Ukara wilayani Ukerewe
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mohammed Abood  (wapili kulia) akiungana na Masheikh katika  sala kwenye mazishi ya wananchi waliofariki dunia katika ajali ya Kivuko cha MV Nyerere kilichozama katika Kisiwa cha Ukara wilayani Ukerewe. Mazishi hayo yaliongozwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa katika kijiji cha Bwisa  kisiwani Bukara.
 Askari wakiweka kaburibi miili ya baadhi ya  wananchi walifariki dunia katika ajali ya Kivuko cha MV Nyerere kilichozama kwenye  kisiwa cha Ukara wilayani Ukerewe wakati wa   mazishi yaliyoongozwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa katika kijiji cha Bwisa kisiwani Bukara,

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.