Moja ya Matenki mapya ya Maji katika Mkoa wa Kusini Unguja yanayotowa huduma hiyo kwa Wananchi wa Wilaya ya Kusini Unguja.
Na. Abdi Shamna
Mamlaka ya
Maji Zanzibar, (ZAWA), Wilaya Kusini Unguja, imeazimia kuyafanyia marekebisho
makubwa matangi ya kuhifadhia maji yaliomo katika ameneo mbali mbali Wilayani
humo, ili kufanikisha dhana ya upatikanaji
wa huduma maji safi na salama kwa
uhakika.
Hatua hiyo
pia inatarajiwa kwenda sambamba na ya ubadilishaji wa mabomba ya kusafirishaji
maji kutoka yale za zamani aina ya Asbestos (saruji) na kuweka ya mipira.
Hayo
yameelezwa na Ofisa wa maji Wilaya ya Kusini Unguja, Hafidh Hassan Mwinyi
katika mkutano uliopitia changamoto mbali mbali zinazowakabili wananchi wa
Wilaya hiyo, kwa lengo la kuzitafutia ufumbuzi wake.
Mkutano huo
uliofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya Kusini Kitogani, umeratibiwa
kwa mashirikiano kati ya Chama cha Waandishi
Habari wanawake (TAMWA) Zanzibar, Jumuiya ya Waandishi wa Habari za Maendeleo
Zanzibar (WAHAMAZA) pamoja na Jumuiya ya Uhifadhi wa msitu wa ngezi Pemba (NGERANECO).
Aidha, mkutano
huo umewashirikisha Watendaji kutoka Serikali za Mitaa Wilaya Kusini Unguja,
Waandishi wa habari kutoka vyombo mbali mbali pamoja na CSO.
Akizungumza
na wadau hao, Mwinyi alisema malengo hayo ya muda mrefu yatahusisha ubadilishaji
wa matangi kadhaa ya kuhifadhia maji Wilayani humo, kutoka yale yaliopo hivi
sasa aina ya Sandarusi na kuweka ya vyuma.
Alisema
hatua hiyo inatokana na matangi mengi
yaliopo hivi sasa kuwa na uwezo mdogo wa kuhifadhi maji kutokana na uchakavu.
Aidha ,alisema
hatua hiyo ni utekelezaji wa muongozo wa
Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO)
lililopiga marufuku matumizi ya mabomba ya Asbestos, kwa maelezo ya kusababisha
ugonjwa wa cancer.
“Kuna
mabomba ya Asbestors katika baadhi ya maeneo, ni hatari na husababisha magonjwa
ya canser, pamoja na WHO kupiga marufuku matumizi ya mabomba hayo, lakini bado
Zanzibar yanatumika katika baadhi ya maeneo’, alisema.
Alisema
pamoja na juhudi kadhaa zinazochukuliwa na Serikali za kuhakikishia Mamlaka
hiyo inawafikishia wananchi wake huduma hiyo muhimu, bado kuna changamoto
mbalimbali, nyingine zikisababishwa na wananchi, ikiwemo matumizi yasio sahihi
ya maji safi na salama.
Alisema
lengo la Serikali ya Mapinduzi ni kuhakikisha wananchi wanapata huduma hiyo
muhimu kwa uhakika na kubainisha kuwepo kwa matumizi makubwa ya maji kwa shughuli za
kilimo, jambo ambalo haliniendani na azma hiyo.
Alisema
matumizi ya maji kwa shughuli za kilimo cha migomba unaofanywa na baadhi ya
wakaazi wa shehiya za Makunduchi, kunadhoofisha juhudi za ZAWA za kuwafikishia
huduma hiyo wananchi.
Alibainisha
kuwa ZAWA imejipanga kuweka utaratibu maalum, ikiwa pamoja na kufunga mita kwa
wananchi wote wanaotumia maji kwa shughuli za kilimo, ikiwa ni hatua ya
kudhibiti upotevu mkubwa wa maji na fedha za umma.
Katika hatau
nyengine, Ofisa huyo alieleza hatari inayowakabili wananchi wa shehiya mbali
mbali za Wilaya hiyo ya kukosa huduma za maji baridi, baada ya visima vingi
kubainika kukumbwa na tatizo la kuingiliwa na maji chumvi, ambapo moja ay
sababu zake ni ufungajj wa mabomba
makubwa.
Mradi wa
Kukuza Uwajibikaji, ulio chini ya usimamizi wa ZANSAP na Ufadhili wa Jumuiya
Ulaya (EU), unatekelezwa katika Wilaya zote 13 za Unguja na Pemba.
Aidha
umewashirikisha Watendaji wa Serikali za Mitaa, Waandishi wa habari na CSO.
No comments:
Post a Comment