Habari za Punde

Chama Cha Mapinduzi Chamnadi Mgombea Wake Ndg Ramadhan Hamza Chande Viwanja Vya Kwahani Unguja.

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Mhe. Salma Kikwete akihutubia wakati wa Mkutano wa Kampeni ya Uchaguzi Mdogo Jimbo la Jangombe Zanzibar, akimuombea Kura Mgombea Uwakilishi wa Jimbo la Jangombe Mhe. Ramadhan Hamza Chande, wakati wa mkutano huo uliofanyika katika viwanja vya Tawi la CCM Kwahani Zanzibar. 

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Mhe. Salma Kikwete akisisitiza jambo wakati wa Mkutano wa Kampeni ya Chama Cha Mapinduzi Jimbo la Jangombe Zanzibar kumuombea Kura Mgombea Uwakilishi wa Jimbo hilo Ndg Ramadhan Hamza Chande katika viwanja vya Kwahani Zanzibar.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dr. Abdallah Juma Mabodi akiwa na Viongozi wa CCM wakifuatilia Mkutano huo wa Kampeni ya Mgombea Uwakilishi Jimbo la Jangombe Zanzibar uliofanyika katika viwanja vya Kwahani Zanzibar.
Mwanachama Mpya wa Chama Cha Mapinduzi akitokea Chama cha CUF Ndg.Salim Mussa Omar wa Gando akizungumza Wakati wa Mkutano huo wa Kampeni ya Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Jangombe Zanzibar akimuombea Kura Mgombea Uwakilishi wa Jimbo hilo kupitia CCM Ndg. Ramadhan Hamza Chande.
Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki Mhe. Abdallah Hasnuu Makame akizungumza wakati wa Mkutano huo wa Kampeni za CCM katika Jimbo la Jangombe uliofanyika katika viwanja vya Kwahani Zanzibar. 
Mbunge wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano kupitia Chama cha CCM Mhe Mwita Waitara akizungumza na Wananchi wa Jimbo la Jangombe katika viwanja vya Kwani wakati wa kumnadi Mgombea wa CCM Uwakilishi Ndg. Ramadhan Hamza Chande.

Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dr. Abdallah Juma Mabodi akimnadi na kumtambulisha Mgombea Uwakilishi Jimbo la Jangombe Ndg. Ramadhan Hamza Chande wakati wa mkutano wa kampeni wa CCM katika viwanja vya Kwahani Zanzibar. No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.