Habari za Punde

Maadhimisho ya Tamasha la Bonaza la Timu ya Ujamaa Uwanja wa Amaan Zanzibar

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Wananamichezo wakati mchezo wa Fainali ya Tamasha la Bonaza la Timu ya Ujmaa na Mlandege mchezo uliuofanyika Uwanja wa Amaan Zanzibar Timu ya Ujamaa imeshinda mchezo huo kwa Bao 1-0.

Na.Othman Khamis OMPR.
Hatimae Bonaza la Timu ya Soka ya Ujamaa kusherehekea Miaka 61 tokea kuasisiwa kwa Kalabu hiyo Kongwe Visiwani Zanzibar limefikia kilele chake katika Uwanja wa Aman Mjini Zanzibar katika Fainali iliyozikutanisha Timu hiyo kwa kupambana na Mlandege.
Katika Mchezo huo wa Fainal ambapo mgeni Rasmi alikuwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif  Ali Iddi Timu ya Soka ya Ujamaa imeibuka Kidedea kwa kuilaza Timu ya Mlandege kwa Magoli 1-0  mchezo uliokuwa wa wastani ukikosa upinzani uliozoeleka kwenye mapambano ya Fainali ya Michezo ya Soka.
Ujamaa iliyovalia Jezi Rangi Manjano imepata ushindu huo kupitia Mchezaji wake Mohamed Simai Vuai  mnamo Dakika ya 41 ya kipindi cha Pili cha Mchezo huo wa Fainali ya Bonaza la Ujamaa.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif alikabidhi zawadi mbali kwa Kipa Bora, Mchezaji bora, Mfungaji Bora na Muamuzi Bora wa mashindao hayo pamoja na cheti Maalum kwa Timu zote zilizoshiriki mashindano hayo.
Hayo ni mashindano ya Pili tokea kuanza kwakeMwaka uliopita kwa Mwaka huu kushirikisha Timu Nane ambazo ni Taifa ya Jang’ombe, Malindi, Mlandege iliyoingia Fainali, Gulioni City, Rasta Zone, Mchangani, Muembe Ladu, Kundemba na wenyeji Ujamaa.
Akizungumza na Wanamichezo hao Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seiof Ali Iddi Kuishukuru na kuipongeza Timu ya Soka ya Ujamaa kwa umahiri wake wa kuandaa Bonaza hilo lililoshirikisha Timu mashuhuri hapa Nchini.
Alisema kiwango cha soka kilichoshuhudiwa kwenye mashindano ya Bonaza hilo yamedhihirisha ukuaji wa Kiwango cha Soka Zanzibar ambacho kimeshuhudiwa na wapenda soka kutokana na Timu ya Soka ya Zanzibar Heroes kuibuka mshindi wa Pili wa Challenge.
Balozi Seif aliwahimiza wanamichezo kuendeleza nidhamu katika michezo  na  mashindano kwa vile mchezo huo unaendeshwa na kuzingatia sheria na Taratibu zilizoridhiwa na Vyama vya Michezo Ulimwenguni kote.
Mapema akimkaribisha Mgeni rasmi kuzungumza na wanamichezo hao Mkuu wa Wilaya ya Mjini Bibi Marina Thomas kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mjini alisema Ujamaa ni Timu yenye Historia kubwa ya kutokana na kuwashirikisha watu mashuhuri hapa Nchini.
Marina alisema ushindi wa Vijana wa Ujamaa Spots Club umethibitisha wazi kwa kuitendea haki Klabu hiyo kutokana na ushindi huo utakaojenga mwnzo mzuri wa kurejea katika hadhi kwa Timu hiyo iliyokuwepo Miaka ya nyuma.
Mchezaji Bora wa mashindano hayo ni Abubakar Ame kutoka Timu ya Mlandege, mfungaji Bora Fahmi Salum kutoka Timu ya Mlandege, Kipa Bora Salula kutoka Timu ya Malindi na Muamuzi Bora ni Kijana Abubakar Khatib wa chuo cha JKU Academy.
Fainali ya mashindano ya Bonaza la Ujamaa Sports Club ilikuwa ifanyike Mnamo Tarehe 22 Septemba lakini iliahirishwa kutokana na Msiba uliowakumba Watanzania kutokana na kuzama kwa Kivuko cha M.V. Nyerere kilichotokea Mkoani Mwanza.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.