Habari za Punde

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Ashiriki Bonaza la Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Ufukwe wa Bwejuu Zanzibar.

Na. Othman Khamis OMPR.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi leo amewaongoza Viongozi na Watendaji wa Taasisi zote zilizo chini ya Ofisi yake katika Bonaza Maalum lililoandaliwa na Ofisi hiyo.
Bonaza hilo lililokuwa la aina yake limelenga kuwapa fursa Watendaji wa Wizara ya Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kufahamiana na kujenga udugu wa Kikazi kufuatia mabadiloko ya Muundo wa Taasisi za Serikali uliofanywa miezi michezche iliyopita.
Balozi Seif aliyeambatana na Mkewe Mama Asha Suleiman Iddi alilizindua Bonaza hilo lililoshirikisha michezo tofauti na kufanyika katika ufukwe wa Hoteli African Sun Sand Sea Bwejuu Mkoa wa Kusini Unguja.
Michezo hiyo ni pamoja na Kuvuta Kamba, Resi za Kuku, Mbio za Magunia, Kula Maandazi, Kupamba Chupa, Soka la Ufukweni ambayo imewajumuisha Watendaji wa Idara na Taasisi zilizo chini ya Ofisi hiyo ambayo ilionekana kuleta Burdani kubwa iliyowafanya Wageni wa Hoteli hiyo kushawishika na kuacha mambo yao.
Akizungumza na Watendaji hao wakati akikabidhi zawadi kwa washindi wa mashindano mbali mbali ya michezo hiyo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema mkusanyiko huo umempa faraja kubwa iliyomuwezesha yeye na Viongozi wenzake kuwafahamu baadhi ya Watendaji wa Ofisi hiyo.
Balozi Seif  Balozib Seif aliwasisitiza Wafanyakazi hao  kuendelea kushirikiana katika majukumu yao ya kazi ya kila siku wakielewa kwamba wao ndio msigi na kiungo muhimu cha Wananchi wakati wanapohitaji huduma za Serikali.
Akifanya mzaha Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwaomba Watendaji hao kujumuika na Familia zao kwenye Bonaza litalofuatia hapo Mwakani ili kutoa fursa miongoni mwa Watedaji hao kufahamiana zaidi jambo ambalo litaongeza mapenzi ya dhati kati yao.
Akimkaribisha Mgeni rasmi katika Bonaza hilo Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mihayo Juma N’hunga alisema Bonaza hilo ni mwanzo mzuri wa kuwakutanisha Wafanyakazi wa Taasisiza Ofisi hizo ili wajenge Utamaduni wa kusaidiana wakati wote wakati wa utekelezaji wa majukumu yao ya Taifa.
Mihayo alisema faida ya mkusanyiko huo imeonekana na Uongozi wa Wizara utaangalia mazingira ya muda mrefu ya kuona Bonaza kama hilo linaendelea kufanyika kila Mwaka.
Mapema Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Bonaza hilo ambae pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira moja ya Idara Mpya iliyofanyiwa mabadiliko na kuwa chini ya Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Bibi  Farhat Ali Abdullah alisema haikuwa kazi rahisi kufanikisha Baonaza hilo kutokana na muda mfupi waliopewa jukumu hilo.
Bibi Farhat aliwapongeza na kuwashukuru wajumbe wote wa Kamati ndogo ndogo zilizounda mjumuiko  wa Kamati Kuu iliyofanikiwa kukamilisha majukumu yao mazito na hatimae Watendaji wote wakaridhika na matokeo ya Kazi hiyo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.