Habari za Punde

Waziri wa Vijana Utamaduni na Michezo Zanzibar Mhe. Balozi Ali Karume (MB) Afunga Tamasha la 'URITHI FESTIVAL' Kijiji cha Makumbusho Jijini Dar es Salaam leo.

Codes
Mgeni Rasmi Mh. Balozi Ali Abeid Karume (MB), Waziri wa Vijana,Utamaduni, Sanaa na Michezo , akitoa hotuba yake rasmi ya kufunga Tamasha la Urithi Festival Jijini Dar es Salaam ambapo alisisitiza kuendelea kudumisha utamaduni wetu kwa kuwa ndio urithi wetu.
Mgeni Rasmi Mh. Balozi Ali Abeid Karume (MB), Waziri wa Vijana,Utamaduni, Sanaa na Michezowa( pili kutoka kushoto) akiwa anaingia katika viwanja vya kijiji cha makumbusho na kupokelewa na ngoma za asili.
Mgeni Rasmi Mh. Balozi Ali Abeid Karume (MB), Waziri wa Vijana,Utamaduni, Sanaa na Michezo (Aliyevaa Suti nyeusi) akitembelea mabanda mbalimbali ya wajasiliamali.
 Mgeni Rasmi Mh. Balozi Ali Abeid Karume (MB), Waziri wa Vijana,Utamaduni, Sanaa na Michezo (aliye vaa  suti nyeusi) akipata maelezo kutoka katika Banda la Waka Shaaban F Kiulah(aliyeshika Mic) Afisa Mkuu wa Misitu kuhusu Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania
  Mgeni Rasmi Mh. Balozi Ali Abeid Karume (MB), Waziri wa Vijana,Utamaduni, Sanaa na Michezo (aliye vaa  suti nyeusi) akipokea zawadi kutoka katika banda la Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania.
 Mgeni Rasmi Mh. Balozi Ali Abeid Karume (MB), Waziri wa Vijana,Utamaduni, Sanaa na Michezo (aliye vaa  suti nyeusi) akipata maelezo kutoka kwa Bw. William Haule Afisa Utalii kutoka Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) kuhusiana na juhudi zinazofanyika kutangaza vivutio nchini Tanzania.
Watu wote wakiwa wamesimama wakati wa Wimbo wa Taifa ukiimbwa kuashiria kufungua Sherehe za kufunga Tamasha la Urithi Festival Jijini Dar es Salaam.
 Mshereheshaji katika kufunga Tamasha la Urithi Festival akitoa maelekezo na kuanza kukaribisha vikundi mbalimbali vya Burudani Kutumbuiza.
 Bendi ya Sisi Tambala wakitumbuiza wakati wa kufunga Tamasha la Urithi katika Kijiji cha Makumbusho, Jijini Dar es Salaam
 Kikundi cha ngoma cha Umoja Shule ya Msingi wakitumbuiza  wakati wa kufunga Tamasha la Urithi katika Kijiji cha Makumbusho, Jijini Dar es Salaam
 Wenyeji kikudi cha ngoma Kijiji cha Makumbusho wakitumbuiza wakati wa kufunga Tamasha la Urithi katika Kijiji cha Makumbusho, Jijini Dar es Salaam
Burudani kabambe zikiendelea
Kikundi cha Sarakati kikonesha vionjo mbalambali wakati wa kufunga Tamasha la Urithi katika Kijiji cha Makumbusho, Jijini Dar es Salaam
 Profesa Audax Mabula, Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya Tamasha la Urithi  Festival, akitoa salam zake wakati wa Kufunga Tamasha la Urithi Festival Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Mh. Jaji Thomas Mihayo, akitoa neno la Salam na kuipongeza kamati ya maandalizi pamoja na wote waliofanikisha Tamasha la Urithi Festival kufanikiwa kwa kiasi kikubwa.
Baadhi ya Wawakilishi wa Balozi Mbalimbali Nchini Tanzania pamoja na wadau wengine wa Utalii wakishuhudia  kufunga Tamasha la Urithi katika Kijiji cha Makumbusho, Jijini Dar es Salaam
 Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania Bi. Devotha Mdachi  (TTB) (aliye simama), Akitoa neno la Shukurani kwa wote waliofanikisha na wananchi wote walioshiriki katika  tamasha la Urithi Festival wakati wa siku zote za maadhimisho hayo yaliyofanyika Jijini Dar es Salaam yakitokea Dodoma na Zanzibar pia kuwaalika watanzania wote katika Maonesho makubwa ya Utalii 'Swahili International Tourism Expo (SITE!) Yatakayo anza ijumaa hii Tarehe 12 hadi 14 katika ukumbi wa kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Msanii Maarufu wa Muziki na mwenye Mashairi ya Kipekee Mrisho Mpoto akitumbuiza katika Tamasha la Urithi, hapa mashairi yake yalijikita zaidi katika kuwaasa watanzania kurudi katika utania wao kwa kuukiza swali la 'wewe ni nani' ? 
Bendi ya wa Hapa hapa wakitumbuiza  wakati wa kufunga Tamasha la Urithi katika Kijiji cha Makumbusho, Jijini Dar es Salaam.
 Mwanamuziki Maarufu wa Muziki wa Singeli Dulla Makabila akitoa burudani ya nguvu wakati wa kufunga Tamasha la Urithi katika Kijiji cha Makumbusho, Jijini Dar es Salaam
 Kikundi Maalum cha Bendi ya watu wenye ulemavu wa kuona  wakitumbuiza  wakati wa kufunga Tamasha la Urithi katika Kijiji cha Makumbusho, Jijini Dar es Salaam.
 Mgeni Rasmi Mh. Balozi Ali Abeid Karume (MB), Waziri wa Vijana,Utamaduni, Sanaa na Michezo (aliyevaa suti nyeusi), akikabidhiwa zawadi ya picha ya Mlima kilimanjaro na  Profesa Audax Mabula, Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya Tamasha la Urithi  Festival
 Mgeni Rasmi Mh. Balozi Ali Abeid Karume (MB), Waziri wa Vijana,Utamaduni, Sanaa na Michezo akionesha picha aliyozawadiwa 
 Mkurugenzi wa Kijiji cha Makumbusho Bi. Agnes Robert akitoa neno la Shukurani wakati wa kufunga Tamasha la Urithi katika Kijiji cha Makumbusho, Jijini Dar es Salaam
 Wakazi wa Jiji la Dar es Salaam pamoja na wananchi wa mikoa ya Jirani wakiwa katika Tamasha la Urithi.
Picha zote na Fredy Njeje

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.