Habari za Punde

Mbunge wa Viti Maalum Kupitia CCM Mhe. Faharia Shomar Amewata Wanawake Kushirikiana Katika Maendeleo.

Na.Takdir Ali -Maelezo Zanzibar.
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mjini Kichama Mh.Faharia Shomar Khamis amewataka akina mama kuhakikisha wanaendelea kukipatia ushindi chama cha Mapinduzi katika uchaguzi mdogo wa jimbo la jangombe unaotarajiwa kufanyika tarehe 27 mwezi huu.
Akizungumza katika Tawi la CCM kwa Alinato ikiwa ni kilelele cha Juma la siku ya Wanawake amesema wanawake wananafasi ya kufanya ushawishi na kuhakikisha chama hicho kinazidi kuimarika.
Aidha Mh.Faharia ameelaani kitendo cha baadhi ya wanaokubali kutumiwa vibaya kwa kujigawa makundi jambo ambalo linaweza kusababisha mtafaruku katika chama.
Amesema suala la Majungu,Fitna na Uhasama haliwezi kuimarisha maendeleo bali ni kurudisha nyuma mikakati iliopangwa na Serikali ya kuwaletea maendeleo wananchi wake kupitia Nyanja mbali mbali ikiwemo vikundi vya Ushirika.
Hata hivyo amewataka Wanawake kuanzisha kampeni ya nyumba kwa nyuma,mtaa kwa mtaa na kitanda kwa kitanda ili kuhakikisha Mgombea aliesimamishwa na Chama Cha Mapinduzi anaibuka kidedea katika Uchaguzi mdogo wa Jimbo la Jangombe.
“Wanawake ni Jeshi kubwa Bwana wee na hata hivyo ni Waume na Watoto wetu iweje tushindwe kuwaenga enga na kufuata tunayoyataka”,Alisema Mbunge Faharia.
Amesema wanawake wanakabiliwa na matatizo ya kijamii ikiwemo tatizo la Ajira,Vikundi vya Ushirika na Mikopo ya kuendesha maisha hivyo hakuna budi kuchaguwa kiongozi wa Chama cha Mapinduzi ili aweze kuwatatulia.
Nae Mwenyekiti Umoja wa Wanawake Tanzania Mkoa wa Mjini kichama Bi Ghanima Sheha Mbwara amewataka Wananchi wa Jimbo la Jangombe kujitokeza kupiga kura na kukiwezesha chama hicho kishinde.
Kilele cha Siku ya Wanawake hufanyika kila mwaka ifikapo Tarehe 4 mwezi wa kumi ambapo kauli mbiyu ya mwaka huu ni wanawake ni chachu ya maendeleo kwa Taifa.
Imetolewa na Idara ya Habari Maelezo Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.