Habari za Punde

MBUNGE WA VWAWA, MHE.JAPHET HASUNGA AGAWA VIFAA VYA MICHEZO VYA MILIONI 17 KWA SHULE ZA SEKONDARI MBOZI

Mbunge wa jimbo la Vwawa ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga akikabidhi seti ya jezi kwa Mwalimu wa michezo Simoni Kalinga   wa Shule ya Sekondari ya Isandula iliyopo wilaya ya Mbozi mkoani Songwe.
Mbunge wa jimbo la Vwawa ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga akipeana mkono wa shukrani kutoka Mwalimu wa michezo,  Aloyce  Mwambungu  wa Shule ya Sekondari ya Msankwi iliyopo wilaya ya Mbozi mkoani Songwe 
Mwanakijiji wa Kijiji cha Mafumbo, Richard Allen akikabidhiwa mpira kwa ajili ya timu ya kijiji hicho wakati Mbunge wa jimbo la Vwawa ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga alipowatembelea kwa ajili ya kuzungumza nao.
Mbunge wa Jimbo la Vwawa amabaye pia ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari ya Isalalo  iliyopo wilaya ya Mbozi mkoani Songwe mara baada ya kuwakabidhi vifaa vya michezo.  

1.   Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari Msankwi iliyopo wilayani Mbozi mkoani Songwe wakimsikiliza Mbunge wa jimbo la   Vwawa ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga wakati alipowatembelea kwa ajili ya kuwakabidhi vaifaa vya michezo.


Na.lusungu helela       

MBUNGE wa Jimbo la Vwawa ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,  Mhe. Japhet Hasunga  amekabidhi seti za jezi pamoja  na mipira yenye zaidi ya  thamani ya sh.milioni 17 katika shule za  Sekondari za kata nne  zilizopo katika jimbo hilo.

Mbali ya kugawa vifaa hivyo, Mhe. Japhet Hasunga ametoa zawadi kwa baadhi ya wanafunzi waliofanya vizuri katika masomo ya Hesabu, Fizikia pamoja na masomo mengine katika mitihani ya taifa  kwa kidato cha pili na cha nne ikiwa ni utekelezaji wa ahadi alizokuwa ameahidi kwa wanafunzi hao
Akikabidhi  vifaa  kwa nyakati tofauti wilayani Mbozi mkoani Songwe katika shule hizo, Mhe. Hasunga  amesema ameamua kutoa vifaa hivyokwa  lengo la kusaidia Serikali katika juhudi za kuinua michezo lakini pia ni sehemu ya kazi zake kama Mbunge
Ameongeza  kuwa michezo licha ya kujenga utimamu wa mwili lakini pia ni ajira huku akitoa mfano kuwa kati ya watu wanaolipwa mishahara mikubwa duniani wachezaji ndio wanaoongoza.
Pia amesema kuwa anatambua kuwa kuna changamoto za kutosha katika michezo hususani vifaa vya michezo Kwa kutambua hilo ameamua kutoa vifaa hivyo huku akiwataka wanafunzi na walimu hao kusimamia vyema
Katika hatua nyingine, Mhe. Hasunga amewataka walimu pamoja na wanafunzi kujenga utamaduni wa kutembelea vivutio vya utalii kwa ajili ya kupumzika na pia ni fursa ya kuweza kujifunza vitu vipya tofauti na vile walivyovizoea. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.