Habari za Punde

Mchezaji Maarufa wa Zanzibar Sabri China Awania Uwakilishi Jimbo la Jangombe Zanzibar. Mkutano wa Uzinduzi wa Kampeni Chama Cha ADA TADEA Viwanja Vya Jumba la Vigae Urusi Jimbo la Jangombe.

 Katibu Mkuu wa Chama Cha ADA TADEA Mhe. Juma Ali Khatib akimtambulisha Mgombea Uwakilishi kupitia Chama cha ADA TADEA Ndg. Sabri China kwa Wananchi wa Jimbo la Jangombe, wakati wa Mkutano wao wa Ufunguzi wa Kampeni uliofanyika katika viwanja vya jumba la vigae urusi jangombe kulia Meneja Kampeni Ndg. Abdi Kassim.

Mgombea Uwakilishi katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Jangombe Zanzibar Ndg. Sabri China akitangaza Sera zake wakati wa mkutano wake wa kwanza wa kampeni katika viwanja vya jumba la vigae Urusi na kuwatangazia neema Vijana na Wazee endapo watampa ridhaa zao kuwawakilisha  katika Baraza la Wawakilishi, na kuondoa kero zote zilizoko katika Jimbo hilo, kulia Meneja Kampeni wake Ndg Abdi Kassin na kushoto Katibu Mkuu wa ADA TADEA Mhe. Juma Ali Khatib.
Katibu Mkuu wa  ADA TADEA Mhe.Juma Ali Khatib akimnadi na kumtambulisha Mgombea wa Uwakilishi katika Uchaguzi Mgodo wa Jimbo la Jangmbe Zanzibar Ndg Sabri Ramadhan China kwa Wananchi wa Jimbo la Jangombe wakati wa Mkutano wao wa Kampeni uliofanyika katika viwanja vya Jumba la Vigae Urusi Jangombe.
Mgombea Uwakilishi kupitia Chama cha ADA TADEA Ndg. Sabri Ramadhin China akizungumza na Wananchi wa Jimbo la Jangombe wakati wa Kampeni yake ya kuomba ridhaa ya kuchagulia kuwa Mwakilishi wa Jimbo hilo na kuwaahidi kuwaletea Nemaa Vijana na Wazee.
Wananchi wa Jimbo la Jangombe wakifuatilia Mkutano wa Kampeni wa Chama cha ADA TADEA uliofanyika katika viwanja vya Jangombe Urusi jumba la vigae.
Katibu Mkuu wa Chama cha ADA TADEA Mhe. Juma Ali Khatib akisisitiza jambo wakati akihutubia katika Mkutano wa Kampeni kumnadi mgombea wake Ndg Sabri Ramadhan China katika viwanja vya Jumba la Vigae Urusi Jangombe.
Mgombea Uwakilishi Jimbo la Jangombe katika Uchaguzi Mdogfo wa Jimbo hilo Ndg. Sabri Ramadhan China akifuatilia Mkutano huo wakati Katibu wa ADA TADEA Mhe. Juma Ali Khatib akihutubiwa katika mkutano huo uliofanyika katika viwanja vya jumba la vigae jangombe urusi.
Mwanachama wa Chama cha ADA TADEA Jimbo la Jangombe akiwa na bendera ya chama hicho wakati wa mkutano wa Kampeni katika viwanja vya Jangombe Urusi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.