Habari za Punde

Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud Akizungumza na Waandishi wa Habari Zanzibar.

Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud akizungumza na Waandishi wa habari wa Vyombo mbalimbali vilioko Zanzibar kuhusiana na kumalizika kwa Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Jang'ombe kwa Amani na Utulivu na kuwapongeza Wananchi wa Jang'ombe kwa utulivu wao.

Na Mwashungi   Tahir            Maelezo     31-10-2018.
MKUU wa Mkoa wa Mjini Magharibi  Mh. Ayoub Mohamed Mahmoud  amewapongeza wananchi wa Jimbo la Jang’ombe  kwa kufanya uchaguzi mdogo wa Jimbo hilo kwa amani na utulivu mkubwa.
Ameyasema hayo Ofisini kwake Vuga wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari kuhusu  uchaguzi mdogo wa Jimbo la hilo uliofanyika tarehe 27.10.2018  ambapo mgombea wa CCM Ramadhan Hamza Chande alishinda  kwa asilimia 90.5 ya kura zilizopigwa.
Alitoa shukurani  za dhati kwa  wananchi wa jimbo la Jangombe  kwa  kuonyesha ustaarabu mkubwa kuanzia  kipindi cha kampeni  hadi wakati wa kupiga kura na hatimae kupatikana mshindi.
Alisema  kabla ya kuanza kwa kampeni wananchi niliwaomba kudumisha amani na wao wamenisikiliza  na kutumia haki yao ya demokrasia  kwa utulivu mkubwa, ningependa kuona ustaarabu kama huo unaendelezwa mpaka kwenye uchuguzi mkuu wa mwaka 2020.
“Tumezowea kuona vurugu wakati wa kipindi cha kampeni na uchaguzi , lakini uchaguzi huu mdogo wa Jimbo la Jang’ombe umekuwa wa amani  nawaomba ustaarabu wa aina hii uendelee kwenye chaguzi nyengine zijazo, “ Alisema Mkuu wa Mkoa.
Aidha alieleza kuridhishwa na usimamizi mzuri wa Tume ya uchaguzi Zanzibar (ZEC),  vyombo vya ulinzi na usalama  pamoja na vyombo vya habari kwa mchango wao mkubwa uliopelekea kufanikisha uchaguzi wa Jimbo hilo ambapo wagombea wote wameridhika na kuyakubali matokeo .
Aliwaeleza wananchi wa Jimbo hilo kuwa uchaguzi umekwisha na  mgombea amepatikana  hivyo watu waendelee na majukumu yao ya kutafuta maisha na kumtakia kheri mwakilishi wa jimbo hilo Ramadhani Hamza Chande.
“Uchaguzi umekwisha  nawaomba wananchi muendelee na kazi zenu za kujiletea maendeleo na sio kukaa vijiweni kuzungumzia siasa,”Alisisitiza Mh.  Ayoub  Mohamed Mahmoud.
Amemtaka mwakilishi huyo mpya  kutekeleza majukumu yake kwa kutumia ilani  ya Chama cha Mapinduzi  kwa  kuwa na mshirikiano na wananchi pamoja na viongozi wenziwe.
caption
Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Ayuob Mohamed Mahamuod akizungumza na Waandishi wa Habari  Ofisini kwake Vuga kuhusu hali ya amani na utulivu wakati wa uchaguzi mdogo wa Jimbo la Jang’ombe uliofanyika tarehe 27/10/2018 (Picha na Kijakazi Abdalla Habari Maelezo)
Imetolewa na Idara ya Habari Maelezo Zanzibar

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.