Habari za Punde

MO DEWJI AWA BILIONEA WA SITA AFRIKA KUTEKWA 2018

KUTEKWA  kwa bilionea kijana nchini Mohamed Dewji ni muendelezo wa matukio yaliyotokea mwaka 2018 hasa katika nchi za Afrika Kusini, Nigeria na Msumbiji.

Jarida la The Citizen limeeleza kuwa tukio kama hilo lilitokea nchini Afrika Kusini ambapo mfanyabiashara  Shiraz Gathoo alitekwa baada ya watekaji kufunga barabara na licha ya kutoa fedha za kumkomboa  alishikiliwa kwa miezi 5.

Jarida la Sunday times la Afrika Kusini April 2018 liliripoti kuwa kwa miaka mitatu zaidi ya wafanyabiashara wakubwa 40 walitekwa nchini humo.

Mwezi Machi mfanyabiashara wa Afrika Kusini afanyaye biashara katika nchi ya Msumbiji Andre Hanekom alitekwa katika hoteli ya Amarula nchini Msumbiji.

Mwezi julai mmiliki wa maduka ya vyakula (supermarket) Liyaqat Ali Parker (35) alitekwa akiwa katika maeneo ya nyumbani kwake huko Afrika Kusini.

Mwezi Julai pia baba wa mchezaji mpira kutoka Nigeria Mikel Obi, chifu Michael Obi alitekwa nyara masaa machache kabla ya mechi ya  Nigeria dhidi ya Argerntina katika msimu wa kombe la dunia. Mikel alieleza kuwa baba yake aliteswa na hiyo ilikuwa ni mara ya pili kabla ya kutekwa mwaka 2011.

Agosti mwaka huu mmiliki wa hoteli  nchini Afrika kusini Sikhumbuzo Mjwara (41) alitekwa na watu wasiojulikana huko Afrika Kusini.

Na leo Agosti 11 Dewji ametekwa nyara na watu wasiojulikana majira ya saa kumi na moja alfajiri katika maeneo ya Colossium hotel, jijini Dar es salaam alipokwenda kwa ajili ya mazoezi.

Polisi wameanza msako na kuimarisha ulinzi katika mipaka mara baada ya kuzipokea taarifa za kupotea kwa bilionea.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.