Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Mkurungenzi Mkuu wa Kampuni ya Pennyroyal Ltd Bw. Brian Thomson, alipowasili katika viwanja vya Kituo cha Watu Wenye Ulemavu wa Jimbo la Shaurimoyo kilichojengwa na Kampuni yake kupitia Mradi wa Best of Zanzibar, wakati wa hafla hiyo ya ufunguzi na kukabidhi Kituo hicho Kwa Wananchi wa Jimbo hilo.baada ya kuweka jiwe la msingi, kulia Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zazibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na kumkabidhi Baskeli mmoja wa Mwananchi Mwenye Ulemavu wa Jimbo la Shaurimoyo baskeli zilizotolewa na Mradi wa Best of Zanzibar, ya Kampuni ya Pennroyal inayojenga Kijiji cha Kitalii Matemwe Zanzibar.hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya Kituo hicho baada ya ufunguzi wake.
Na.Mwandishi Wetu.
Katika
juhudi za kuendeleza kuboresha maisha ya Wazanzibari, Blue Amber kupitia
kitengo chake cha kusaidia jamii Best of Zanzibar kimeungana na Viongozi wa Chama Cha Walemavu kwa kujenga kituo cha Watu wenye UlemavuShaurimoyo.
Katika
jimbo la Shaurimoyo kuna baadhi ya wananchi walemavu wanaojishughulisha na
miradi tofauti ya biashara ili kujipatia kipato na kuwasaidia katika mahitaji
yao ya kila siku. Viongozi wa chama cha walemavu na Mhe. Hamza Juma walitaka
kuboresha mazingira wanayofanyia
biashara,
hivyo walikutana na Mkurungenzi Mkuu wa Kampuni ya Pennyroyal Ltd Bw.
Brian Thomson na kumwelezea mahitaji ya Walemavu katika jimbo la Shaurimoyo.
Bw. Brian Thomson hakusita na kukubali kujenga kituo hicho cha walemavu ili
kusaidia wanajamii hao. Kituo hicho kitawezesha vijana na wazee kupata mafunzo
mbali mbali na kuwawezesha walemavu hao kufanya biashara zao.
“Napenda
kuleta mabadiliko chanya duniani, japo hata kwa mtu Mmoja. Naamini unapo
msaidia mtu Mmoja anaweza saidipia familia na jamii inayo mzunguka. Kwa sababu
hii, Pennyroyal Ltd inafanya kazi kwa karibu na jamii ya waleavu ili kuleta
mabadiliko kwa watoto, wanaume na wanawake wasiojiweza.” Alisema Bw. Brian
Thomson Mkurungenzi
Mkuu wa Pennyroyal Ltd. “Nataka kuweka msisitizo kwa sekta
binafsi na wawekezaji waliopo Zanzibar kuungana nasi nakujenga vituo kama hivi
katika majimbo mengine na kuwafikia wananchi wengi zaidi Zanzibar.” Aliongezea
Bw.Thomson.
Meneja
wa programu ya Best of Zanzibar Bi. Aminata Keita alisema “Kama Kampuni
tunaamini kwamba tukiandaa mazingira mazuri ya kufanya kazi na kusaidia watu wasiojiweza tunawapa nafasi nzuri ya kujiendeleza na kujifunza biashara mbali
mbali zitakazo wawezesha kupata ajira na kujikwamua kiuchumi. Hivyo basi naomba
viongozi na wanajamii wote watunze kituo hichi ili kusaidia kizazi kijacho na
kuleta maendeleo endelevu. Juhudi zetu kwa pamoja zitasaidia kuwafikia wengi
wasiojiweza katika jamii, tunataka mradi huu uguse maisha ya watoto na watu wazima,ndio mana tunahitaji kila mmoja aupe uzito ili ufanikiwe.
Nae
Mwakilishi wa jimbo hilo Bwana Hamza Hassan Juma, alitoa wito kwa Wawekezaji
wengine na wasamaria wema kuunga mkono juhudi za Best of Zanzibar. “Tunaishukuru Best of Zanzibar kwa msaada huu na tunaishukuru Pennyroyal Ltd kama Mwekezaji
kwa jitihada zao kubwa katika kuboresha maisha ya wasiojiweza. Kuna wengi wanaohitaji katika jimbo letu ambao kwa Pennyroyal na Serikali peke yao
hawawezi kuwamaliza, tunahitaji wadau wengine kuungana nao katika juhudi hizi
za kuboresha maisha kwa wasiojiweza.”
Kituo
hicho kilifunguliwa rasmi na Makamo wa Pili wa Rais Zanzibar, Balozi Seif Ali
Iddi. Balozi Seif aliwapongeza Pennyroyal kwa kazi nzuri wanayofanya na kuwa
mfano wa kuigwa na Wawekezaji wengine. “ Tunashukuru sana msaada kutoka Best of
Zanzibar na mchango wao mkubwa kwenye elimu na kuwawezesha wanajamii.”
Alimalizia Balozi Seif Pamoja
na ufunguzi wa jengo hilo, Mr. Brian Thomson amewalipia Bima ya Afya watoto 50
walemavu na kuchangia Milioni moja taslim kwenye Account ya Manedeleo ya Walemavu. Kwa kuongezea, Best of Zanzibar imetoa baskeli nne za walemavu, vifaa
vya ofisini kama kompyuta, printa, mashine ya fotokopi, lamineshen na
nyenginezo ili kurahisisha kuendeleza vizuri ofisi hiyo.
Kwa
maelezo zaidi kuhusu Best of Zanzibar unaweza
kututembelea kupitia: www.best-of-zanzibar.com
na Blue Amber Zanzibar unaweza kutembelea: www.blueamberzanzibar.com
No comments:
Post a Comment