Habari za Punde

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Eng.Masauni Azishukia Shule Zenye Magari Mabovu Zanzibar.


Mkurugenzi  wa Taasisi  inayojishughulisha  na  masuala  ya  usalama  barabarani ,Pily  Hamisi  Layda (kushoto)  akimkabidhi  Naibu  Waziri  wa  Mambo  ya  Ndani ya Nchi, ambae pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi  Hamad  Masauni, mpango kazi wa  Kampeni  Maalumu  ya Usalama  Barabarani  na  Udhibiti wa Ajali iliyozinduliwa  katika Uwanja wa Skuli ya Jang’ombe, leo  Visiwani Zanzibar
Naibu  Waziri  wa  Mambo  ya  Ndani ya Nchi, ambae pia ni Mwenyekiti wa Baraza  la  Taifa  la  Usalama  Barabarani, Mhandisi  Hamad Masauni, akimkabidhi Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Jang’ombe, Tiffy Mustafa (kushoto), moja ya kikoti maalumu watakachokua wanavaa wanafunzi watakaoteuliwa  kuwasaidia  wenzao kuvuka barabara  baada ya kuzindua Kampeni  Maalumu  ya  Usalama  Barabarani  na  Udhibiti  wa  Ajali katika Uwanja wa Skuli ya Jang’ombe, leo Visiwani Zanzibar.
Naibu  Waziri  wa  Mambo  ya  Ndani ya Nchi, ambae pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama  Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza wakati  ya  Uzinduzi  wa  Kampeni  Maalumu  ya  Usalama  Barabarani na Udhibiti  wa  Ajali  katika  Uwanja  wa Skuli ya Jang’ombe, leo Visiwani Zanzibar.
Mwanafunzi  wa  Shule  ya  Msingi  Jang’ombe, Aisha Abdallah Haji, akiuliza swali  linalohusiana  na  uvukaji  wa  barabara kwa watu wenye ulemavu wakati wa  Uzinduzi  wa  Kampeni  Maalumu  ya Usalama Barabarani na Udhibiti wa Ajali katika  Uwanja  wa  Skuli  ya  Jang’ombe, iliyozinduliwa  leo Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambae  pia  ni  Mwenyekiti  wa  Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni (hayupo pichani), Visiwani Zanzibar
Wanafunzi  wakifurahia  jambo wakati  Naibu  Waziri  wa  Mambo  ya  Ndani ya Nchi, ambae pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni (hayupo pichani), akizungumza  baada  ya  kuzindua Kampeni  Maalumu  ya  Usalama  Barabarani  na  Udhibiti wa Ajali  katika Uwanja wa Skuli ya Jang’ombe, leo  Visiwani Zanzibar.
 Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

Na Mwandishi Wetu, Zanzibar
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambae pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni, amewatadharisha wamiliki wa shule  zinazotumia magari mabovu kubebea wanafunzi ikiwa ni kinyume na sheria za usalama barabarani hali ambayo inaweza kupelekea ajali.

Akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Kampeni Maalumu  ya Usalama Barabarani na Udhibiti wa Ajali katika Uwanja wa Skuli ya Jang’ombe, Naibu Waziri Masauni aliwataka wamiliki wa shule  kuhakikisha wanatumia mabasi imara ili kuepusha ajali na kuwaasa madereva wa magari hayo kufuata sheria za barabarani

“Wamiliki wa shule wanatakiwa wafuate sheria kwa kuacha  kutumia mabasi mabovu na  kujaza wanafunzi kupita kiasi na tutatumia kikosi cha usalama barabarani kuhakikisha wanafunzi wanakua salama muda wote wakiwa wanaenda shule na kurudi nyumbani.

“Nawaagiza askari wa usalama barabarani kusimamia sheria ili wamiliki watakaokiuka sharia hizo waweze kuchukuliwa hatua pamoja na madereva watakaobainika kuendesha magari mabovu ambayo ni hatarishi kwa wanafunzi,” alisema Masauni

Akitoa ripoti ya matukio ya ajali za barabarani Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Polisi Zanzibar, Shukuru Amir Ally alisema jumla ya ajali 229 zimeripotiwa ndani ya mwaka huu tofauti na mwaka 2017 ambapo jumla ya ajali 391 zikiripotiwa huku akitoa siri ya kupungua kwa ajali hizo ni ushirikiano wanaoupata kutoka kwa wadau wa usalama barabarani.

Akisoma risala ya uzinduzi huo Mkurugenzi wa Taasisi inayojishughulisha na masuala ya usalama barabarani ya New Vision, Pily Hamis Ladya alisema wamedhamiria kufikia mikoa yote ya Zanzibar na katika awamu hii ya kwanza wanaanza na shule kumi huku akiahidi kuzifikia shule zote katika kutoa elimu ya usalama barabarani kwa wanafunzi.

“Tunategemea kutoa elimu hii ya usalama barabarani ili kuweza kuwaepusha na kuwalinda wanafunzi wetu na majanga ya barabarani ili waweze kwenda shule na kurudi nyumbani salama,” alisema.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.