Habari za Punde

TFF Wateuwa Kamati Mpya Itakayosimamisha Soka la Zanzibar.


Shirikisho la Soka nchini Tanzania (TFF) limeteua kamati mpya ndogo ya wajumbe 10 watakaosimamia soka la Zanzibar kwa muda mfupi.

Akizungumza na Waandishi wa Habari katika Ukumbi wa V.I.P wa uwanja wa Amaan Raisi wa Shirikisho hilo Wallace Karia amesema kamati hiyo itakuwa na jukumu la kusimamia upatikanaji wa Katiba ya ZFA, kushughulikia shughuli zote za ZFA za Kikatiba pamoja na kutayarisha Uchaguzi mpya kwaajili ya kupatikana viongozi wapya wa ZFA.

Karia amesema kamati hiyo wameiunda baada ya vikao vya muda mrefu baina ya pande zote na kupata muafaka wa TFF kuunda kamati hiyo ambayo itafanya kazi zake hadi Novemba 30 mwaka huu.

Kuhusu suala la kamati ya iliounda mrajisi wa vyama vya michezo Karia amesema kamati hiyo kwa sasa haitofanya kazi tena baada ya TFF kuteuwa kamati hiyo ndogo na mazungumzo baina ya TFF na mrajisi wa vyama vya michezo Zanzibar yalifanyika na kufahamiana vizuri.

Kamati hiyo imeundwa na wajumbe kumi wafuatao :- Mwalim Ali Mwalim (Mwenyekiti), Mohamed Ali Hilali “Tedy” (Katibu), Ahmada Haji Shaabani (Mjumbe) , Rashidi Tamimu Khalfan (mjumbe), Ikram Omar Sleman (mjumbe), Salum Ubwa Nassor (Mjumbe), Rajabu Juma Mtumweni (Ujumbe), Mzee Ali Abdalla (mjumbe), Khamisi Abdalla Saidi (Mjumbe) na Mzee Ali Mzee (Mjumbe).

Baada ya kuundwa Kamati hiyo imezifuta kamati nyengine ndogo ndogo ikiwemo Kamati ya Soka la wanawake, Kamati ya Soka la Vijana (Central Taifa), Kamati ya Uchaguzi pamoja na Kamati ya  Rufaa na Usuluhishi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.