Habari za Punde

Wajumbe Baraza la Wawakilishi wapatiwa mafunzo ya uzazi wa mpango

  KATIBU Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar akizungumza na kuwakaribisha Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi katika Mafunzu ya siku mbili ya Uzazi wa Mpango yalioandaliwa na Wizara ya Afya kupitia Kitengo shirikishi cha Afya ya Mama na Mtoto na Shirika linaloshughulikia idadi ya Watu Duniani UNFPA katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Mbweni Zanzibar.
 KIKUNDI cha maigizo kutoka Tumbatu (TUMBATU HEALTH ASSOCIACTION) kikitoa burdani ya igizo la uzazi wa mpango mbele ya wajumbe wa Baraza hilo pichani hawapo katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Mbweni Zanzibar.
 SPIKA wa Baraza la Wawakilishi Zubeir Ali Maulid, wa pili kulia Naibu Spika Mgeni Hassan Juma,Mwenyekiti wa Baraza Mwanaasha Khamis Juma na Naibu Waziri wa Afya Harusi Said Suleiman wakifuaatilia kwa Umakini igizo lililokua likioneshwa na kikundi cha maigizo kutoka Tumbatu .
 MENEJA Kitengo cha Afya ya Mama na Mtoto Dkt. Ali Omar Ali akiwasilisha mada ya Afya ya Uzazi na Ujinsia na Mchango wake katika kuboresha Afya ya Mama na Mtoto kwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar katika khafla iliofanyika katika Ukumbi mdogo wa Baraza hilko Chukwani Zanzibar.
 SHEKHE Abdalla Talib Abdalla akiwasilisha mada Uislamu na Uzazi wa Mpango kwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar katika khafla iliofanyika katika Ukumbi mdogo wa Baraza hilko Chukwani Zanzibar.
 WAJUMBE wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar na Maafisa kutoka Wizara ya Afya na Shirika linaloshughulikia Idadi ya Watu Duniani waliohudhuria katika Mafunzo hayo yaliofanyika katika Ukumbi mdogo wa Baraza hilko Chukwani Zanzibar.
 WAJUMBE wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar na Maafisa kutoka Wizara ya Afya na Shirika linaloshughulikia Idadi ya Watu Duniani waliohudhuria katika Mafunzo hayo yaliofanyika katika Ukumbi mdogo wa Baraza hilko Chukwani Zanzibar.

SPIKA wa Baraza la Wawakilishi Zubeir Ali Maulid akifungua  Mafunzu ya siku mbili ya Uzazi wa Mpango yalioandaliwa na Wizara ya Afya kupitia Kitengo shirikishi cha Afya ya Mama na Mtoto na kushirikiana na Shirika linaloshughulikia idadi ya Watu Duniani UNFPA katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Mbweni Zanzibar.

Picha na Abdalla Omar Maelezo - Zanzibar 

Na Kijakazi Abdalla     Maelezo    
SPIKA wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Zubeir Ali Maulid amesema kama kutakuwa na matumizi sahihi ya njia za kisasa za uzazi wa mpangilio kuna uwezekano mkubwa wa kupunguza vifo vinavyotokana na asilimia 30.
Hayo ameyasema huko Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Chukwani wakati akifungua mkutano wa kuhamasisha matumizi ya njia za uzazi wa mpangilio kwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar.
Alisema kuwa ripoti zinaonesha kuwa wanawake 800 hufariki kila siku duniani kutokana na matatizo ya ujauzito wakati wa kujifungua na baada ya kujifungua.
Aidha alisema kuwa asilimia 20 ya wanawake hupata matatizo makubwa kabla ya kufariki na asilimia 90 ya vifo hivyo hutokea katika nchi zinazoendelea.
Hata hivyo Mhe.Zubeir alisema kwa upande wa Zanzibar huduma za uzazi wa mpangilio bado si ya kuridhisha na takwimu zinaonesha ya mwaka 2015/16 ni asilimia 14 ya kina mama wenye uwezo wa kuzaa wanatumia njia hizo kwa sasa.
Alisema kuwa kiwango hicho ni kidogo sana tulichojiwekea na lengo ni kufikia asilimia 20 hadi ifikapo 2020 katika dira ya maendeleo  na mkakati 111 wa sekta ya afya.
Aidha alisema kuwa matumizi madogo ya njia za kisasa za uzazi wa mpangilio hali hii inaweka hatarini maisha ya mama na mtoto ya uzazi wa papo kwa papo na kunaongezeka kwa umasikini na kudumaza kwa ukuaji wa maendeleo katika nchi.
Hata hivyo alisema kuwa mbali na sababu hizo pia Zanzibar na Nchi nyingi zinahusisha na Imani za mitazamo ya kidini,mila na desturi na ushiriki mdogo kwa wanaume kwa huduma za uzazi wa mpangilio.
Sambamba na hayo Mhe,Spika alisema kuwa kina mama wengi wamekuwa wakipata vikwazo katika kutoa maamuzi sahihi ya njia za uzazi wa mpangilio na hali hupelekea kuwa mzigo kwa familia na Serikali kwa kuongezeka huduma za kijamii ikiwemo afya na elimu.
Hata hivyo alisema kuwa kwa upande wa vifo hali hairidhishi katika nchi nyingi za kiafrika ambapo wanawake 276 kati ya vizazi hai 100,000 wanafariki kila mwaka na watoto 28 katika kila watoto 1000 hufariki kila mwaka.
Hata hivyo ameziomba asasi za kijamii,viongozi wa dini,wanasiasa kuhamisha matumizi ya njia za uzazi wa mpango ili kupunguza vifo vya kina mama na watoto nchini.
Nae Katibu Mkuu Wizara ya Afya Asha Abdalla amesema kuwa lengo la kuweka mafunzo hayo kwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi ni kuwapa uwelewa na wananchi juu yakufuata njia sahihi za uzazi wa mpango ili kupunguza tatizo la vifo vya kina mama na watoto.
Hata hivyo alimeitaka jamii kutoa mashirikiano kwa pamoja ili lengo la kuwepo njia ya matumizi uzazi wa mpango lifikiwe ili kasi ya ukuaji wa watu iendane na ukuaji wa uchumi nchini.

Imetolewa na Idara ya Habari Maelezo Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.