Habari za Punde

*GAVANA SHILATU ATAKA MRADI WA MAENDELEO USIOKAMILIKA VYEMA USIPOKELEWE*


Na Mwandishi wetu, Mihambwe
Gavana Mihambwe, Emmanuel Shilatu amesisitiza jukumu kubwa la viongozi wa Serikali ni kuhakikisha utekelezaji wa ilani ya uchaguzi unafanyika kwa kuhakikisha miradi inayopokelewa ni ile iliyokamilika vyema.

Gavana Shilatu aliyasema hayo wakati alipotembelea mradi wa ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa katika Shule ya Sekondari Mkoreha ili kujionea hatua iliyofikiwa.

*Tarafa ya Mihambwe tunatekeleza, Viongozi wote wa Serikali tuna jukumu kubwa la kuhakikisha tunasimamia na kutekeleza vyema ilani ya uchaguzi ya CCM kwa kuhakikisha miradi ya kimaendeleo inayokabidhiwa ina ubora unaolingana na thamani ya pesa. Hivyo mradi wa maendeleo usiokamilika vyema usipokelewe."* alisema Gavana Shilatu.

Gavana Shilatu  alisifu hatua iliyofikiwa ya mradi huo wa ujenzi na kusisitiza madarasa hayo yakamilike haraka ili yaanze kutumika mara moja.

*"Napongeza hatua iliyofikiwa. Kuanza kutumika kwa madarasa haya yatakidhi mahitaji yaliyopo ambayo yameongezeka kutokana na fursa ya elimu bure na bora ambayo Serikali ya CCM inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Magufuli inatoa. Hivyo Madarasa haya yakamilishwe vyema mara moja na yaanze kutumika mapema iwezekanavyo."* alisisitiza Gavana Shilatu.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.