Habari za Punde

Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Azindua Jeshi la USU.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikagua gwaride wakati wa sherehe za uzinduzi wa Jeshi USU la Wanyapori na Misitu iliyofanyika Fort Ikoma Serengeti mkoani Mara.
Jeshi USU la Wanyamapori na Misitu likipita kwa ukakamavu mbele ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (hayupo pichani) wakati wa sherehe za uzinduzi wa jeshi hilo zilizofanyika Fort Ikoma Serengeti mkoani Mara.
Jeshi  USU la Wanyamapori na Misitu likionyesha picha za Viongozi wakubwa wawili Mwalimu Julius K. Nyerere (kulia) kama ishara ya mpambanaji wa kusimamia rasilimali zetu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kama mtekelezaji katika kuhakikisha rasilimali zetu zinalindwa na kufaidisha Wananchi wa Tanzania  na picha za wanyama zinaashiria wanyama wakubwa watano ambao ndio kivutio zaidi duniani na wamekuwa kwenye hatari ya kutoweka wakati wa sherehe za uzinduzi wa jeshi hilo zilizofanyika Fort Ikoma Serengeti mkoani Mara. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi bendera Mkurugenzi Mkuu wa Hifahi za Taifa (TANAPA), Dkt. Allan Kijazi kama ishara ya uzinduzi na kuanza kufanya kazi rasmi kwa jeshi la USU leo wakati wa sherehe za uzinduzi wa Jeshi  USU la Wanyapori na Misitu iliyofanyika Fort Ikoma Serengeti mkoani Mara.
Jeshi USU la Wanyamapori na Misitu likipita kwa mwendo wa pole mbele ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (hayupo pichani) wakati wa sherehe za uzinduzi wa jeshi hilo zilizofanyika Fort Ikoma Serengeti mkoani Mara.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.