Habari za Punde

Mchezo wa Kirafiki wa Timu ya Yanga na Namungo Uwanja wa Majaliwa Ruangwa Zatoka Sare ya Bao 1 - 1.

Mshambuliaji wa Yanga, Maka Edward   (kulia) akipiga  mpira huku akizuiwa na  beki wa Namungo, Hashim Manyanya katika mechi ya kirafiki iliyochezwa kwenye uwanja wa Majaliwa katika Halmashauri ya wilaya ya Ruangwa
Andrew Vincent wa Yanga akizuia mpira kwa kichwa huku akizongwa na  Reliant Lusajo wa Namungo katika mechi ya kirafiki iliyochezwa kwenye uwanja wa Majaliwa katika Halmashauri ya wilaya ya Rungwa
Deus Kaseke wa Yanga akimili mpira katika mechi ya kirafiki kati ya timu yake na Namungo iliyochezwa kwenye uwanja wa Majaliwa katika Halmashauri ya wilaya ya Ruangwa, Novemba 18, 2018. Timu hizo zilitoka sare  1 – 1
Reliant Lusajo wa Namungo FC  (kushoto) akimiliki mpira huku akizongwa na Juma Abdul wa Yanga katika mechi ya kirafiki iliyochezwa kwenye Uwanja wa Majaliwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa
Kiungo na mshambuliaji wa Yanga, Thaban Kamusoko akijaribu kufunga kwa tikitaka bila mafanikio mbele ya beki wa Namungo FC, Juma Jamal akimkabili katika mechi ya kirafiki iliyochezwa kwenye uwanja wa Majaliwa katika Halmashauri ya wilaya ya Ruangwa Novemba 18, 2018. Kushoto ni Kipa wa Namungo FC,  Adam Oseja.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wapenzi wa mpira wa miguu baada ya kukagua timu za Yanga na Namungo zilizocheza mechi ya kirafiki kwenye uwanja wa Majaliwa katika Halmashauri ya wilaya ya Ruangwa Novemba 18, 2018. Kulia kwake ni mkewe Mary , wapili kushoto ni Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga na kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi. Timu hizo zilitoka sare 1-1. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.