Habari za Punde

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi Akiwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Baada ya Kumaliza Ziara Yake Nchini Oman.

 
Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Mh. Ayoub Mohamed Mahmoud akimlaki Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kwe ye Uwana wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Aman Karume Zanzibar aliyetokea Nchini Oman kwa ziara Maalum ya Wiki Moja.
Balozi Seif akisalimiana na Naibi Waziri Wizara ya Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mihayo Juma N’hunga alipowasili Uwanja wa ndege wa Zanzibar akitokea Nchini Oman.Kulia ya Mh. Mihayo ni Mkuu wa Wialay ay Mjini Bibi Marina Thomas, Meja wa Manispaa ya Magharibi “B” Mstahiki Maabad Alui Maulid na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Nd. Shaaban Seif.
Balozi Seif akielekea Chumba cha Watu Mashuhuri {VIP} Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Zanzibar kwa mapumziko mafupi akitokea Nchini Oman kwa Ziara Maalum.
Picha na – OMPR - ZNZ.

Na.Othman Khamis Ame, OMPR.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amerejea Zanzibar leo mchana kwa Ndege  ya Shirika la Ndege la Oman {Omar Air} akitokea  Nchini Oman kwa ziara Maalum.
Balozi Seif  Ali Iddi katika safari hiyo Maalum alifuatana na Mkewe Mama Asha Suleiman Iddi pamoja na baadhi ya Wasaidizi wake  wa kazi.
Kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Aman Karume Zanzibar Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alipokea na Viongozi mbali mbali wa Serikali pamoja na baadhi ya Maafisa Waandamizi wa Serikali.
Balozi Seif  na Ujumbe aliofuatana nao aliondoka  Zanzibar Tarehe 27 Oktoba Mwaka 2018.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.