Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, Azungumza na Ujumbe wa Jumuiya ya Kaunti za Pwani Nchini Kenya.


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Magavana wa Jumuiya za Kaunti za  Pwani Nchini Kenya katika ukumbi wa Hoteli ya Inter Continental Jijini Nairobi Kenya kulia Balozi wa Tanzania Nchini Kenya Dkt. Pindi Chana na kushoto Balozi wa Kenya Nchini Tanzania Mhe. Dan Kazungu.

Na.Suzan Kunambi Nairobi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein amekutana na kufanya mazungumzo na Jumuiya ya Magavana wa kaunti za ukanda wa Pwani ya Kenya,katika ukumbi wa mikutano wa hotel ya Intercontinental mjini Nairobi na kusema Zanzibar ipo tayari kuimarisha ushirikiano uliopo baina ya pande mbili hizo.

Lengo la mkutano huo nikujadili  mambo mbali  yenye mnasaba na maisha na shughuli za  watu wa ukanda wa pwani. Katika mkutano huo, pande mbili zilijadilia  mafanikio na changamoto mbali mbali ambazo zinadhorotosha shughuli za kiuchumi na  juhudi zilizopo za kuimarisha uhusiano huo.

Viongozi wa Jumuiya hiyo walitoa pongezi kwa Dk. Shein kwa kutenga muda maalum wa kukutana nao  na kujadili mambo mbali mbali  kwa lengo la kuimarisha ustawi wa wanachi wa eno hilo.

Katika kikao hicho Dk.Shein alitoa fursa  kwa  kila mmoja wa Gavana wa kaunti hizo  kuelezea   mambo ambayo angependa kuelezea katika kikao hicho kwa kuzingatia malengo ya mkutano huo.  Vile vile, alitoa fursa kwa viongozi wa Zanzibar aliokuwa amefuatana nao kutoa ufafanuzi na maelezo  ya ziada  kwa kuzingatia hoja zilitolewa na magavana wa akaunti hizo.

Miongoni mwa mambo yaliyojadiliwa ni haja ya kumarisha uhusiano baina ya Watu wa Zanzibar  na watu Ukanda wa Pwani pamoja na watu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Watu wa Kenya kwa jumla, pia  pande mbili hizo, zilijadili njia bora za kuimarisha sekta ya uvuvi ambayo ni shughuli muhimu ya kiuchumi kwa  wananchi wa eneo hilo.

Viongozi hao  walijadili juu ya umuhimu wa kukaa pamoja ili kuzifanyia kazi changamoto ziliiyopo zikiwemo za kukamatwa wavuvi wadogo wadogo wa pande zote mbili  wenye kuvua katika mipaka  ya Jamhuri ya Kenya na Tanzania.

Viongozi wa Jumuiya hiyo, waliompongeza Dk Shein kwa juhudi zake za kuimarisha huduma za meli baina ya Zanzibar na Mombasa kwa kutumia meli ya Mv Mapinduzi 2. Walisema kwamba ni vyema hivi sasa huduma za usafiri wa baharini zikaimarishwa  hatua ambayo itaimarisha uhusiano wa kindugu uliopo pamoja na kuimarisha sekta ya utalii.

Kuhusu sekta ya utalii, viongozi hao wa   ukanda wa pwani walisema kwamba una rasilimali muhimu kwa kuimarisha sekta ya utalii ambazo bado hazitumika ipasayo. Vile vile, walishauri kamba itakuwa ni vyema ikiwa Zanzibar itaendeleza aina mpya ya utalii “ Utalii wa vita vya Pili vya Dunia”  ambao umezingatia uhifadhi wa maeneo yenye historia inayohusiana vita vya dunia pamoja na kuwatembeza wageni katika maeneo hayo, ambayo pia yapo mengi Zanzibar.

Vile vile, walisema itakuwa ni vyema pande mbili hizo kushirikiana katika kutoa mafunzo ya utalii kupitia Chuo Kikuu cha Taifa (SUZA) Zanzibar na taasisi mbali mbali zinafundisha utalii nchini Kenya.

Walipendeaza vile vile  haja ya kukaa pamoja kwa ajili ya kujadili njia bora itayaweza kuandika upya historia ya ukanda wa Pwani kwa kuwashirikisha wataalamu wa historia waliopo nchini Kenya na Tanzania .

Aidha  walisema itakuwa ni vyema ikiwa pande mbili hizo zitashirikiana katika kuimarisha zao la  karosho, ambapo hadi sasa wakulima wa Kenya hawafanyi vizuri, katika kilimo hicho. Walisema kwamba wananchi wa Kenya  wako tayari kujifunza kwa ndugu zao  wa Tanzaia ambao wamepiga hatua katika kilimo cha korosho.

Vile vile, walieza kwamba hivi sasa wananchi wengi wa ukanda wa Pwani nchini Kenya wameanza kujishghulisha na uzalishaji wa zao mwani. Kwa hivyo walisema  kwamba wangependa kuona kwamba wakulima hao wanakuja kujifunza kwa wenzao wa  Zanzibar ambao wana uzeofu mkubwa na wemepiga hatua katika uzalishaji wa zao hilo.

Mhe Rais,akitolea ufafanuzi changamoto ya kukamatwa kwa wavuvi wa  wanaokamatwa kwa kuvua katika  maeneo ya nje ya mipaka ya nchi zao,alisema ni muhimu kwa wavuvi hao na wananchi wengine wakazingatia sheria na taratibu zilizowekwa ili kukabiliana na changamoto hiyo.

Akitoa maelezo baada ya kusikiliza hoja zilizotolewa na magavana hao Dk. Shein,alisema kwamba amefurahi kusia hoja hizo ambazo zinaguza moja kwa moja uchumi wa bahari ambao ndio uliowakutanisha kwa pamoja mjini Nairobi. Alifananua na kukubali na kuzisitiza juu ya haja ya kufuatia utekelezaji wa mambo yaliyojadilwa katika kikao.

Ipo haja ya kuendelea kutolewa elimu zaidi kwa wavuvi wa pande hizo mbili pamoja na  kuwepo kwa vikao rasmi vya mara kwa mara kwa viongozi  ili kuweza kuzitatua changamoto mbali mbali zinazozojitokeza”Alisema Dk. Shein.

Dk. Shein aliwashukuru magavana hao kwa uwamuzi wao wa kuomba kukutana nae na kusema mkutano huo umefungua ukurasa mpya wa ushikiano katika njanja mbali mbali ikiwemo Utalii,Usafiri,  bandari, biashara, Uvuvi na kilimo cha mwani,  mapambano dhidi ya dawa za kelevya pamoja na usalama katika ukanda wa pwani wa Afrika Mashariki.

Akitoa shukrani kwa Mhe Rais kabla ya kufunga  kikao hicho , Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kaunti  hizo sita za ukanda huo wa Pwani Mhe  Salim M.Mvurya ambae pia ni Gavana wa Kwale, alisema jumuiya yake  tayari kushirikiana na Tanzania katika kutafuta suluhu ya wavuvi hasa wadogo wadogo wanaokamatwa wakiwa katika shughuli za kujitafutia riziki, jambo ambalo kurudisha nyuma juhudi zao za kujikomboa na umaskini wa kipato.

Mapema wakitolea ufafanuzi wa masuala yaliyoelezwa na Magavana hao ,Waziri wa Kilimo, Maliasili,Mifugo na Uvuvi wa Zanzibar Mhe Rashid Ali Juma,alisema kuwa matumizi mazuri ya rasilimali za baharini yanaweza yakasaidia katika kutatua tatizo la ajira kwa vijana, kwa hivyo ni vyema pande mbili hizo zikaimalisha ushikiano katika sekta hizo muhimu.

Nae Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Abdallah Ulega,alizungumzia suala la korosho na kusema Tanzania imepiga hatua kubwa katika kilimo hicho na kuwakaribisha magavana hao kwenda kujifunza na kubadilishana uzoefu.

Kwa upande wa mshauri wa Rais Ushirikiano wa Kimataifa Fedha na Uchumi Balozi Mohamed  Ramia alishauri kuanzishwe ushirikiano baina ya kaunti hizo sita za ukanda wa Pwani  na Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais  Tawala za Mikoa,Serikali za Mitaa na   Idara Maalum za SMZ,kupita wakuu wa Mikoa  ili kuweza kufuatilia na kutekeleza mambo yaliyojadiliwa na kupangwa katika kikao hicho.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.