Habari za Punde

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi Alipongeza Shrika la Umeme Zanzibar ZECO.

Meneja Mkuu wa Shirika la Umeme Zanzibar {ZECO} Nd. Hassan Ali Hassan Kushoto akimkabidhi sampuli ya Hundi ya shilingi 50,000,000/- Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kwa ajili ya kuchangia mfuko wa sherehe za Mapinduzi.
r.

Picha na – OMPR – ZNZ.
 Balozi Seif kati kati akiupongeza Uongozi wa Shrika la Umeme Zanzibar {ZECO} kwa uamuzi wake wa kusaidi nguvu za Serikali katika kufanikisha vyema Maadhimisho ya Sherehe za Kutimia Miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Picha na – OMPR – ZNZ.
Na.Othman Khamis OMPR.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alipokea Hundi yenye thamani ya Shilingi Milioni 50,000,000/- iliyotolewa na Uongozi wa Shirika la Umeme Zanzibar {ZECO} kwa ajili ya kuchangia mfuko wa Sherehe za Mapinduzi zinazofikia Kilele chake Kisiwani Pemba.
Meneja Mkuu wa Shirika hilo Ndugu Hassan Ali Hassan alimueleza Balozi Seif kwamba Uongozi wa Shirika lake umefikia hatua hiyo baada ya kuona uzito wa sherehe hizo ambapo Serikali inalazimika kuungwa mkono ili kufanikisha vyema maadhimisho ya sherehe hizo.
Akipokea Hundi ya Fedha hizo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ameupongeza na Kuushukuru Uongozi wa ZECO kwa uamuzi wake wa kuiongezea nguvu Serikali katika kufanikisha malengo ya Sherehe hizo.
Balozi Seif alisema Sherehe za Mapinduzi ni za Wazanzibari wote. Hivyo kitendo cha ZECO kuchangia kwake kinastahiki kuigwa na Taasisi nyengine za Umma na hata zile binafsi.
“ Leo mmeanza  nyinyi ZECO mnaoonekana kufungua njia. Kesho tutarajie Taasisi nyengine kuiga mfano huo muhimu na mzuri katika mazingira ya Taifa letu linalohitajika kujengwa na sisi sote”. Alisema Balozi Seif.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwapongeza wataalamu na Watendaji wa Shirika la Umeme Zanzibar kwa uwajibikaji wao wa kusambaza huduma za Umeme katika kila kona ya Visiwa vya Zanzibar jambo ambalo huleta faraja kwa Jamii nzima.
Balozi Seif alisema inapendeza kuona hata Visiwa vidogo vidogo vimeanza kupata huduma hiyo muhimu ambayo kwa maisha ya sasa sio hanasa bali ni nyenzo muhimu inayosaidia Wananchi katika harakati zao za Kiuchumi na Maendeleo za kila siku.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.