Habari za Punde

Naibu Waziri Mhe Kanyasu Akutana na Kufanya Mazungumzo na Balozi wa Uingereza Nchini Tanzania.

Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Sarah Cooke mapema leo Alhamisi Januari 10, 2019 amekutana na kufanya mazungumzo na   Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu katika ofisi ndogo ya Wizara ya Maliasili na Utalii. Mpingo House jijini Dar es Salaam ambapo pamoja na mambo mengine wamejadili namna ya kukabiliana na tatizo la ujangili wa tembo pamoja na mikakati ya kukuza  utalii nchini.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu(katikati)  akizungumza na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Sarah Cooke (kulia) kabla ya kuagana naye wakati alipotembelewa ofisini kwake jijini Dar es Salaam.
 Balozi wa Uingereza nchini Tanzania,Sarah Cooke  (katikati) akizungumza na  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu(kulia) uhusiana  na mikakati mbalimbali ya kukabailiana na tatizo la ujangili wa tembo nchini mapema leo  ofisini kwake Mpingo House  jijini Dar es Salaam
(Picha na Lusungu Helela -MNRT)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.