MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella akizungumza na
wajasiriamali kwenye soko la Muheza mjini wilayani humo ambako
alikwenda kuwahimiza umuhimu wa kuwa na vitambulisho vya ujasiriamali
ili waweze kutambulika rasmi na kufanya shughuli zao
MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella akizungumza na wajasiriamali
kwenye soko la Muheza mjini wilayani humo ambako alikwenda kuwahimiza
umuhimu wa kuwa na vitambulisho vya ujasiriamali ili waweze kutambulika
rasmi na kufanya shughuli zao kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Muheza
Mhandisi Mwanasha Tumbo
MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella kushoto akigawa
vitambulisho kwa wajasiriamali wilayani Muheza wakati alipokwenda
kuhamasisha wajasiriamali wasiokuwa kwenye sekta rasmi ambapo
kwa wilaya ya Muheza wamepewa vitambulisho 3000 ambavyo vitagawiwa kwa
wajasiriamali wilayani humo
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine
Shigella akikagua bidhaa za mjasiriamali wilayani Muheza wakati
alipokwenda kuhamasisha umuhimu wa wao kuwa na vitambulisho ili waweze
kutambulika
MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella kulia akiwa na Mkuu wa
wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo wakitembelea maeneo
mbalimbali Muheza mjini kuhamasisha wajasiriamali kuwa na vitambulisho
vilivyotolewa na Rais Dkt John Magufuli ili waweze kutambulika
rasmi
MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella kushoto akiwagawa
vitambulisho kwa wajasiriamali wilayani Muheza wakati alipokwenda
kuwahamasisha
MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella kushoto akisisitiza jambo
kwa wajasiriamali wilayani Muheza kabla ya kuwakabidhi vitambulisho
MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella kushoto akimsikiliza kwa umakini mmoja wa wajasiriamali wilayani Muheza ambaye aliuliza swali wakati wa uhamasishaji huo uliofanywa na mkuu huyo wa mkoa |
Sehemu ya maafisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA wilayani
Muheza wakiendelea na zoezi la kuandikisha wajasiriamali kwa ajili ya
kupatiwa vitambulisho wakati wa uhamasishaji huo uliofanywa na Mkuu wa
Mkoa wa Tanga Martine Shigella leo
MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella kulia akimsikiliza kwa
umakini Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo mara baada ya
kumaliza uhamasishaji wa wajasiriamali kuchangamkia fursa ya
vitambulisho vilivyotolewa na Rais Dkt John Magufuli
Sehemu ya wajasiriamali wakifuatilia maelezo ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga
Martine Shigella ambaye hayupo pichani
MKUU wa Mkoa wa
Tanga Martine Shigella amewahamisha wajasiriamali wilayani Muheza
kuchangamkia fursa ya vitambulisho vilivyotolewa na Rais Dkt John
Magufuli ili waweze kutambulika rasmi na kufanya shughuli zao.
Huku akisisitiza dhamira ya kuendesha misako kuanzia siku ya
Jumatano na ambao watakutwa hawana kitambulisho hicho watakuwa
wanahusika ufanyaji wa biashara haramu za magendo ambazo
hazitambuliki.
Akizungumza mara baada ya kuwakabidhi
vitambulisho kwa wajasiriamali wilayani Muheza,RC Shigella alisema
wanapaswa kuchangamkia fursa hiyo muhimu kwa ajili ya kutambulika ili
waweze kufanya kazi zao vema ambapo kwa wilaya ya Muheza vitagawiwa
kwa wajasiriamali 3000.
“Lakini niwaambie kwamba
kitambulisho cha Uraia,Leseni ya gari na kile cha kupigia kura isiwe
kigezo cha kukufanya ushindwe kupata kitambulisho cha
mjasiriamali…unachotakiwa kufanya kama hauna unaandika jina lao mahali
unapoishi namba yako ya simu unasaidiwa utakapokamilisha hivyo
vyengine utawaletea”Alisema RC Shigella.
Aidha pia
aliwataka wajasiriamali wasiokuwa kwenye sekta rasmi kujitokeza kwa
wingi ili waweze kupatiwa vitambulisho hivyo ili waweze kutambulika na
hatimaye kuweza kuondaka na usumbufu wakati wakiendesha biashara zao
“Ndugu zangu Rais wetu aliona wajasiramali na
wafanyabiashara wanapata shida na usumbufu hivyo akaona ili kuweza
kuondoa hilo akaona kuwepo na utaratibu wa vitambulisho”
Alisema kwamba vitambulisho hivyo vinatolewa kwa yoyote asiyekuwa na
TIN namba na ambaye alipi kodi hivyo kuwataka kuona umuhimu wa
vitambulisho hivyo ili waweze kuendesha biashara zao.
Naye
kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo
alisema wataendelea kuhamasisha ili wajasiriamali wengine waweze
kuchangamkia fursa ya kuwa na vitambulisho hiyo.
No comments:
Post a Comment