Waziri wa Habari Utamaduni
Sanaa na Michezo Mheshimiwa Dkt.Harrison Mwakyembe akitoa maelekezo kwa Idara ya Utamaduni kufika katika himaya ya
Chifu Kingalu kwa ajili ya kukusanya taarifa muhimu za utamaduni usiyoshikika
zenye historia ya zaidi ya miaka mia nne kwa ajili ya kuhifadhi na kutangaza
kwa mashirika ya kimataifa leo katika
kijiji cha Kinole Mkoani Morogoro katika hafla ya makabidhiano ya zana za
kijadi za Chifu Kingalu Mwanabanzi wa Kwanza zilizokuwazimeibiwa na kurudishwa
katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Morogoro .
Chifu Kingalu
Mwanabanzi XV (wa kumi) akizungumza wakati wa sherehe za makabidhiano ya zana
za jadi za chifu huyo wa kwanza zilizokuwa zimeibiwa tangu kipindi cha ukoloni
leo katika kijiji cha Kinole na kurejeshwa hivi karibuni katika Ofisi ya Mkuu
wa Wilaya ya Morogoro wa kwanza kulia ni Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na
Michezo Mhe.Dkt Harrison Mwakyembe.
Waziri wa Habari
Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt.Harrison Mwakyembe (wa kwanza kulia)
akishuhudia baadhi ya zana za jadi zilizokuwa zimepotea kwa zaidi ya
miaka mia moja na kurejeshwa hivi
karibuni zikionyeshwa kwa jamii
ya Waluguru (hawapo pichani) na Mjukuu wa Chifu Kingalu Bw.Hamis Athumani leo
wakati wa sherehe za makabidhiano ya zana hizo
zilizofanyika katika himaya ya chifu huyo katika kijiji cha Kinole Kata
ya Mtamba Mkoani Morogoro.
Chifu Kingalu
Mwanabanzi wa XV akitoa maelezo kuhusu sanamu hiyo iliyoko kulia kwakwe kuwa ni mfano wa mama mzazi wa Chifu Kingalu wa Kwanza na alieleza kuwa
sanamu hiyo inanguvu nyingi ikiwa ni pamoja na uwezo wa kuzungumza na pia ni moja ya zana hizo
zilizokuwa zimeibiwa na kurejeshwa, wakati wa sherehe ya makabidhiano ya zana
hizo leo katika kijiji cha Kinole Mkoani Morogoro.
Waziri wa Habari
Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt.Harrison Mwakyembe akisimikwa na Chifu Kingalu Mwanabanzi wa XV, kuwa Chifu
Mkazi miongoni mwa Machifu wa Baraza lake leo wakati wa hafla ya makabidhiano
ya zana za Kijadi za Chifu huyo zilizokuwa zimepotea kwa zaidi ya miaka mia
moja iliyofanyika leo katika kijiji cha Kinole Mkoani Morogoro.
Waziri wa Habari
Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt.Harrison Mwakyembe (wanne kulia) na Chifu
Kingalu Mwanabanzi wa XV (wanne kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na
viongozi wa baraza la chifu huyo mara baada ya sherehe za makabidhiano ya zana
za kijadi ziizokuwa zimepotea kwa zaidi ya miaka mia moja na kurejeshwa hivi
karibuni, ambapo sherehe hizo zimefanyika leo katika Kijiji cha Kinole Mkoani
Morogoro , (watatu kulia) ni Kaimu Mkuu wa Mkoa ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya
Ulanga Mhe.Ngollo Malenya.
Na. Anitha Jonas –
WHUSM,Kinole.Morogoro.
Waziri wa Utamaduni
Sanaa na Michezo Mheshimiwa Dkt.Harrison Mwakyembe ameigiza Kurugenzi
ya Idara ya Utamaduni katika Wizara yake kufika katika himaya ya Chifu
Kingalu Mwanabanzi wa XV (kumi na tano) wiki ijayo kwa ajili ya kukusanya
taarifa zote zinahusu urithi wa utamaduni huo usiyoshikika wenye histori ya
zaidi ya miaka mia nne iliyopita.
Mheshimiwa Dkt.Mwakyembe
ameyasema hayo leo katika Kijiji cha Kinole Kata ya Mtamba Mkoani Morogoro katika
hafla ya Makabidhiano ya Mali Kale za Chifu Kingalu Mwana Msumi wa kwanza wa
kuanzia mwaka 1600 ambaye zana zake za jadi ziliibiwa na katika mazingira ya
kutatanisha na kurushishwa hivi karibuni.
“Kwa historia ya
uongozi huu wa kijadi wenye zaidi ya miaka mia nne kama nilivyoelezwa hapa na
kuonyeshwa baadhi ya vitu ninaona kuna
kila sababu ya himaya hii ya Chifu kujengwa sehemu ya Makumbusho na taarifa
zitakazo kuja kuchukuliwa na watendaji wangu wa wizara nitazisimamia na kuzipeleka katika mashirika mbalimbali ya
Kimataifa ambayo yako tayari kufanya kazi na sisi na kuhifadhi zana hizi za asili,”alisema Mhe.Dkt.Mwakyembe.
Akiendelea kuzungumza
katika hafla hiyo Waziri huyo mwanye dhamana na masuala ya utamaduni alitoa
wito kwa viongozi wote wa kijadi nchini kuhakikisha wanakuwa mbele katika
kulinda na kuhifadhi misitu na mali kale kwani ndiyo urithi wa utamaduni kwani
kwa kufanya hivyo kutasaidia kuongeza chachu ya utalii wa kiutamaduni.
Naye Mmoja wa Dada wa
Chifu Kingalu Bibi.Gaudensia Lukwele aliyesoma risala kwa niaba ya Chifu
Kingalu XV alitoa ombi kwa Wizara hiyo yenye dhamana na masuala ya
Utamaduni kuanza kutambua na kuweka
katika rejesta ya wizara machifu wa Tanzania
na mali kale zao pamoja na ujuzi wa asili wa jamii zao katika makarama
mbalimbali.
“Tunaomba serikali
itambue na kuiwezesha miliki ya Chifu
Kingalu iwe sehemu ya makumbusho itakayo tembelewa na watu wa ndani na nje ya
nchi kukidhi haja ya uchifu ikiwa ni pamoja na kuboresha miundombinu ya
barabara iliiweze kufikika kwa urahisi na miliki hii niya kuvutia na ya kipekee
duniani na isiyohamishika,’’alisema Bibi.Lukwele kwa niaba ya chifu.
Pamoja na hayo nae
Mjukuu wa Chifu Kingalu Mwanamfuko wa Kumi Bw.Semeni Kingalu alieleza kuwa zana
hizo za matambiko ya asili ya Chifu Kingalu zinauhusiano mkubwa wa
kiutamaduni baina ya nguvu za kimila na
uhifadhi wa mazingira,ikiwemo uhifadhi wa misitu na uoto wa asili,vyanzo vya
maji,hali ya hewa ,mvua na utajiri.
“Zana hizo zinatambulika
kwa majina ,uhalisia wake na ikiwemo kumuenzi kiongozi wa kwanza Chifu Kingalu
ambaye hajafa mpaka sasa hivi mwenye zaidi ya miaka mia nne na uongozi wake wa
kimila upo katika mikoa ya Morogoro,Tanga,Pwani na Dar es Salaam,”alisema
Mjukuu wa Chifu Kingalu.
Hata hivyo katika
hafla hiyo viongozi hao wa jamii ya kichifu walisisitiza suala la jamii ya
watanzania kudumisha mila asilia za makabila ya kiafrika kuziheshimu kwa
kutokuwa na mmomonyoko wa maadili pamoja na desturi za kijadi zenye misingi ya
amani,umoja,mshikamano,kuheshimiana na utunzaji wa mazingira.
No comments:
Post a Comment