Habari za Punde

Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu Aweka Jiwe la Msingi Madarasa Sita ya Shule ya Msingi Mwakidila Jijini Tanga.

Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu na Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoa wa Tanga  akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Jiwe la Msingi kwenye madarasa sita ya shule ya Msingi Mwakidila Jijini Tanga yaliyofadhiliwa na Ubalozi wa Japani nchini kutokana na jitihada zake kuhakikisha changamoto za uhaba wa vyumba vya madarasa vinakwisha kwenye Jiji hilo kwa kushirikiana na wadau na wananchi kulia ni Mkuu wa wilaya ya Tanga.


Na.Assenga Oscar.Tanga.
WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee wa Watoto na Mbunge wa Viti  Maalumu Mkoani Tanga Ummy Mwalimu leo ameweka jiwe la Msingi kwenye  madarasa sita shule ya Msingi Mwakidila Jijini Tanga yaliyofadhiliwa na  Ubalozi wa Japani nchini.

Ujenzi wa madarasa hayo unatokana na jitihada kubwa zilizofanywa na Waziri Ummy kuhakikisha anashirikiana na wananchi wa Jiji la Tanga kuweza  kuzipatia ufumbuzi changamoto zinazoikabili sekta ya elimu ikiwemo ujenzi  wa madarasa kwa shule zenye uhaba ili kuwawezesha wanafunzi kusoma bila  kuwepo kwa vikwazo.

Mradi wa ujenzi huo uliofadhiliwa na Ubalozi wa Japani nchini Tanzania  kupitia shirika la TAWODE (Tanga Women Development Initiative) una thamani  ya shilingi Milioni 179,777,898.00 pamoja na madawati 180 mpaka kumalika kwake.

Akizungumza katika halfa hiyo Waziri Ummy alisema baada ya kuwepo kwa uhaba  wa vyumba vya madarasa ambapo darasa moja kwenye shule hiyo lilikuwa  likikaa wanafunzi 166 ndipo alipoamua kuweza kuishughulikia changamoto hiyo  kwa vitendo na kufanikiwa kupata ufadhili huo ambao umewezesha ujenzi huo.

Halfa hiyo ilihudhuriwa na Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa,Naibu Meya wa Jiji la Tanga Mohamed Haniue,madiwani  na  viongozi mbalimbali wakiwemo wa idara ya Elimu Jiji hilo wakiwemo viongozi  wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Tanga wananchi,walimu na wanafunzi.

Alisema kwa serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Magufuli  inastahili kupongeza kila wakati kutokana na kuanzisha sera ya elimu bure  ambayo matokeo yake yameanza kuonekana kutokana na kuwepo kwa ongezeko la  uandikishaji wa wanafunzi wanaoingia darasa la kwanza Jijini Tanga mwaka  huu.

“Kwa mujibu wa takwimu za Jiji la Tanga uandikishaji wa wanafunzi wa shule  ya Msingi umeongezeka kutoka mwaka 2015 watoto 8495 hadi watoto 10345 mwaka  2018 na ongezeko hilo sio kwa sababu watu wanazaa sana kutokana na kwa  mujibu wa takwimu zao kiwango cha wanawake kuzaa watoto kimepungua sana  kuliko zamani mwanamke anaweza kuzaa watoto mpaka saba.

Alisema kwamba kwa sasa mwananke mmoja anaweza kuzaa watoto kati ya watano  na hao walikuwa majumbani na walikuwa hawaendi shule kutokana na  kukwamishwa na ada na michango mbalimbali ambayo awamu hii imeamua kuiondoa  na hivyo wananchi kuweza kuwapeleka watoto wao shuleni kutokana na sera ya  elimu bure bila malipo.

Aidha aliwataka wananchi wa mkoa wa Tanga kuendelea kumuunga mkono Rais  Magufuli ili aweze kuendelea kuijenga Tanzania mpya ya viwanda kwa vitendo  kutokana na kazi kubwa anayoifanya kuhakikisha watanzania wanapata  maendeleo

“Ndugu zangu wana Tanga Rais wetu Mh Dkt John Mgufuli amefanya kazi kubwa  sana kuhakikisha watoto wanapata elimu na kila mwezi amekuwa akitoa milioni 54 kwa shule za msingi Jiji la Tanga na Milioni 55 kwa shule za Sekondari  kwa ajili ya kuhakikisha watoto wanasoma bila malipo hivyo niwaambieni  tutamlipa kwa kazi kubwa na mazuri kutokana na mambo makubwa aliyoyafanya
tumuonyeshe kwa vitendo kwenye serikali za mitaa kwamba tupo pamoja  naye”Alisema Waziri Ummy.

Naye kwa upande wake Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji alipongeza  juhudi kubwa zinazofanywa na Waziri Ummy ambako kwa Jiji hilo wanajivunia  sana kuwa na kiongozi kama yeye kutokana na namna alivyojitoa kusaidia  maendeleo huku akimuhaidi kuchangia tiles kwa madarasa hayo sita.

Alisema kwa kipindi cha mwaka 2018 waliandikisha wanafunzi darasa la kwanza  asilimia 121 ya lengo ambalo walikadiria kuandikisha akwani walikaadiria  wanafunzi 8506 na waliweza kuandikisha10345 hali inayonyesha mwitiko mkubwa  wananchi kuwapeleka waoto shule.

Alisema hali hiyo miaka ya nyuma hakuwepo huku akieleza mwitikio huo  wananchi watahakikisha wanaweka miundombinu sambamba na watoto  wanaondikishwa kwenye shule hizo ili waweze kupata sehemu ya kusomea.

Hata hivyo alitoa wito kwa wazazi na wananchi kushirikiana na serikali  kujenga miundombinu ya shule ili kuweza kuhakikisha wanafunzi  wanaondikishwa kujiunga na darasa la kwanza wanapata fursa ya kusoma

“Lakini pia nimshukuru Rais kwa kuleta mpango wa elimu bila malipo kwani  kwa kipindi cha miaka miwili shule za msingi zimepokea milioni 984.8 kama ruzuku inayokwenda moja kwa moja kwa shule kutekeleza mpango elimu bila  malipo…2017/2018 milioni 656.8 ziliwekwenda moja kwa moja shule za msingi  na mwaka 2018/2019 wamepokea kuanzia desemba milioni 325 mpango huu umeweza kuwasaidia shule zao kwenye mambo mengi “Alisema.

Pia alisifu jitihada kubwa zinazofanywa na Waziri Ummy kuhakikisha  anakuwa mstariu wa mbele kutatua changamoto za wananchi licha na kuwa na majukumu makubwa lakini umekuwa akitujali watu wa Tang.

Mkurugenzi huyo alisema katika Jij la Tanga kuna shule za msingi 104 za  serikali 79 changamoto nyingi za hali ya miundombinu shule za msingi za  Jiji la Tanga mahitaji ya vyumba vya madarasa 1251 lakini vilivyopo 710  upungufu ni vyumba 541.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.