Habari za Punde

Waziri wa Kazi Uwezeshaji Wzee Wanawake na Watoto Zanzibar Mhe. Maudline Castico Azindua Mradi wa Ufugaji wa Kuku Zanzibar.

Na Mwashungi Tahir. Maelezo - Zanzibar.
Makamo wa Pili wa Raisi wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi  amewataka Vijana kutumia fursa zinazotolewa na Serikali ili waweze kufaidika kwa kupata ajira na kujiongzea kipato cha kuweza kuendesha maisha yao ya kil;a siku.
Alisema Ilani ya Chama cha Mapinduzi inataka kuwezeshwa wananchi kiuchumi ikiwemo vijana ili waweze kujiletea maendeleo.
Akizungumza kwa niaba yake Waziri wa Kazi,Uwezeshaji wanawake na Watoto Maudline Cyrus Castico huko kwenye uwanja wa Mapinduzi Square Kisonge katika uzinduzi wa mradi wa Uwezeshaji Ajira na kujiongezea kipato kwa vijana kupitia ufugaji wa kuku.
Aidha alisema mradi huo umeanzishwa na Mkuu  wa Mkoa Mjini Magharibi Ayoub Mohamed Mahmoud  kwa lengo la kupunguza umasikini kwa vijana na kupata kujishughulisha na miradi ili kujiepusha na kuepukana na mambo maovu ambayo yatawaharibia mustakbali wa dira  ya maisha yao.
Amewataka vijana hao kuitumia fursa hiyo ili waweze kufaidika kwa kupata ajira  itakayoweza kuwaongezea kipato katika maisha  yao ikiwa ni utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi katika kuitumikia wananchi wake na kuwaletea maendeleo.
“Nataka vijana muichangamkie fursa zinazotoka serikalini kupitia katika Wizara ya Kazi Uwezeshaji Wanawake na Watoto kwa lengo la kuwaletea maendeleo mazuri katika maisha yenu”, alisema Waziri Castico.
Pia alisema anampongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein kwa jinsi anavyowatilia mkazo vijana kwa kuwapatia fursa mbali mbali ili waweze kujikwamua kimaisha wao pamoja na familia zao.
Hivyo aliwaomba vijana hao kuzidisha mashirikiano katika mradi huo kutumia fursa hiyo kwa wale waliopata elimu waweze kuwa walimu kwa  wenzao na kuwapatia elimu hiyo ya ufugaji kuku ili na wao waweze kutumia fursa hizo watazoelekezwa .
Vile vile aliipongeza asasi ya mimi na wewe kwa hatua wanazochukuwa kwa kuimarisha wananchi wake wakiwemo vijana kwa kuwawezesha kiuchumi na kimaendeleo katika Mkoa huo .
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa mjini Magharibi Ayoub Mohamed Mahmoud ambae pia ni Mlezi wa Mradi huo alisema dhamira kubwa ya kuwakusanya vijana kuwa pahala pamoja na kuwawezesha ni kutaka kujikwamua kimaisha kwa kuwaanzishia miradi mbali mbali ikiwemo ya ufugaji wa kuku.
Pia alisema kufanya hivyo tunakusudia kupunguza umasikini kwa vijana ambao wao ndio tegemeo la kesho katika utendaji wa kazi zao za kujiongeze kipato.
Akisoma risala katika uzinduzi huo Msimamizi wa Mradi wa Ufugaji kuku Rashid Muhammed Othmani alisema amempongeza Mkuu huyo wa Mkoa kwa kuazisha Mradi huo ambao utawezesha kuwakwamua na tatizo la umasikini lililodumu kwa muda mrefu kwa vijana na kuwaomba viongozi wengine kuiga mfano kama huo.
Hata hivyo amesema juhudi anazozichukua katika kuwakwamua vijana kumewawezesha vijana kujikwamua kiuchumi jambo ambalo litawaweka katika mazingira rafiki na kuwa wazalendo , wapenda amani  na kuilinda nchi yao.
Aidha alisema juhudi hizo zinazochukuliwa  zinawanufaisha vijana walio  wengi na kusababisha kuachana na vitendo vilivyo viovu na kuweza kufuata miongozo na maadili  ya  mambo yaliyo mema na kupelekea Taifa kusonga mbele kwa kuwa na vijana waliyo madhubuti.
Mradi huo wa ufugaji wa kuku aina ya Saso unasimamiwa na kampuni ya Silverland kutoka Iringa na umewapa mafunzo vijana kumi na mbili  na kuifikisha walimu kwa vijana wenzao wafikao 300 na tayari  wanavifaranga vya kuku mia tisa na hamsini 9,500 katika kituo cha malezi ya vifaranga vya kuku huko Mwachealale shehia ya Mbaleni Wilaya ya Kaskazini B.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.