Habari za Punde

Mwenyekiti wa CCM.Mhe Rais Dkt.John Magufuli Atembelea Kituo Cha Television Cha Channel Ten na Radio Magic Fm Jijini Dar es Salaam.Febuary,5,2019.

Mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Mkewe Mama Janeth Magufguli na Mkurugenzi mtendaji African Media Group (AMG) Jaffari Haniu wakimsikiliza mtangazaji wa kituo cha Channel Ten Hanifa Roy alipotembelea kuangalia utendaji kazi wa Vituo vya Televisheni na Radio vinavyomilikiwa na Chama cha Mapinduzi CCM. Wakati wa Maadhimisho ya Miaka 42 ya CCM. Jijini Dar es Salaam.Febuari 5,2019. 
Mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akizungumzana Wafanyakazi na Watangazaji wa Channel Ten na Radio Magic Fm,  alipotembelea kuangalia utendaji kazi wa Vituo vya Televisheni na Radio vya African Media Group vinavyomilikiwa na Chama cha Mapinduzi CCM. Wakati wa Maadhimisho ya Miaka 42 ya CCM. Jijini Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Bi. Diana Mwakatundu ambaye ni Mlemavu aliwapokuwa akizungumza na Wananchi mbalimbali waliokuwa nje ya Ofisi za Channel Ten na Radio Magic Fm,  alipotembelea kuangalia utendaji kazi wa Vituo vya Televisheni na Radio vya African Media Group vinavyomilikiwa na Chama cha Mapinduzi CCM. Wakati wa Maadhimisho ya Miaka 42 ya CCM. Jijini Dar es Salaam. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wananchi mbalimbali waliokuwa nje ya Ofisi za Channel Ten na Radio Magic Fm,  alipotembelea kuangalia utendaji kazi wa Vituo vya Televisheni na Radio vya African Media Group vinavyomilikiwa na Chama cha Mapinduzi CCM. Wakati wa Maadhimisho ya Miaka 42 ya CCM. Jijini Dar es Salaam

Mama Janeth Magufuli Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimu Wananchi mbalimbali waliokuwa nje ya Ofisi za Channel Ten na Radio Magic Fm,  walipotembelea kuangalia utendaji kazi wa Vituo vya Televisheni na Radio vya African Media Group vinavyomilikiwa na Chama cha Mapinduzi CCM. Wakati wa Maadhimisho ya Miaka 42 ya CCM. Jijini Dar es Salaam. 

Wananchi mbalimbali wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli aliwapokuwa akizungumza nao Wananchi hao waliokuwa nje ya Ofisi za Channel Ten na Radio Magic Fm,  alipotembelea kuangalia utendaji kazi wa Vituo vya Televisheni na Radio vya African Media Group vinavyomilikiwa na Chama cha Mapinduzi CCM. Wakati wa Maadhimisho ya Miaka 42 ya CCM. Jijini Dar es Salaam. Febuari 5, 2019.
                                                                          Picha na Ikulu.
NA K-VIS BLOG.
RAIS Dkt. John Pombe Magufuli, “ameimwagi” shilingi milioni 200 runinga ya Channel Ten iliyo chini ya kampuni ya African Media Group, ambayo kwa sasa imechukuliwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Rais Magufuli ambaye amefanya ziara ya kushitukiza kwenye studio za Channel Ten zilizoko eneo la Kisutu jijini Dar es Salaam, leo Februari 5, 2019, amesema fedha hizo atazikabidhi kesho.
Mmoja wa wafanyakazi wa Channel Ten alisema, kituo hicho kinakabiliwa na uhaba wa camera na uchakavu wa vifaa mbalimbali, na kwamba zinahitajika camera 6 za kisasa ili kuongeza ufanisi katika shughuli za kituo hicho.
Baada ya madai hayo zilifanyika hesabu za haraka haraka na ikaonekana kila camera moja inapatikana kwa thamani ya dola za Kimarekani 7,000 na kwa camera sita zingehitajika Dola 42,000 karibu shulingi milioni 90.
“Mimi nitawapatia shilingi milioni 100 na nitawaongezea shilingi milioni 100 nyingine na kuwa Milioni 200.” Alisema Rais Magufuli na kuonya, fedha hizo zitumike kwa lengo lililokusudiwa na si vinginevyo.
Kampuni ya African Media Group (AMG), inamiliki vituo vya televisheni vya CTN, DTV na Channel Ten na Radio Magic FM, imechukuliwa na CCM.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.