Habari za Punde

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Tanzania Mhe. Mpina Luhaga Azungumza na Kutoa Maagizo Mazito.


WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina
Na. John .Mapepele, Mpwapwa
WAZIRI waMifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina amemuagiza Mkurugenzi waUtafiti, Mafunzo na Ugani kuandaa haraka kanuni na mwongozo utakaosimamia kuanzia uvunaji wa mbegu, uuzaji, usambazaji na uhimilishaji na uhamilisha mifugo kabla ya mwezi Machi mwaka huu ili kuwadhibiti madalali wote wanaokwenda kuwaumiza wananchi kwakutumia kivuli cha Serikali.

Akizungumza mara baada ya kutembelea Mradi wa uzalishaji kwa kutumia teknolojia ya viinitete na uhawilishaji (MOET) unaotekelezwa na TaasisiyaUtafitiwaMifugo (TALIRI) Kituo cha Mpwampwa mkoani Dodoma, Waziri Mpina alisema watanzania wajivunie mradi huo ambao niwa kwanza katika ukanda wa Afrika Mashariki na kati.

Alisema kupatikana kwa teknolojiaya MOET kumeiwezesha Tanzania kuwa na njia tatu za kuboresha Koosafu ya mifugoa mbapo ni njia ya asili ya kutumia madume bora, uhimilishaji (AI) na Uhamilishaji (MOET) ambapo itachochea mageuzi makubwa ya uboreshaji wakoosafu ya mifugo ambayo itaongeza uzalishaji wa maziwa, nyama, ngozi na mazao mengine ya mifugo.

Aidha aliagiza kuwa kila ifikapo mwezi Machi ya kila mwaka idara yake iwe imepeleka ajenda za kufanyiwa utafiti kwenye Taasisi ya Utafiti wa Mifugo ili kupata matokeo ya tafiti ambazo watanzania wanaumiza vichwa kutafuta ufumbuzi wa matatizo yanayowakabili na kuweka utaratibu wakupokea tafiti kutoka nje ya nchi.

Pia amemwagiza Mkurugenzi huyo waUtafiti, Mafunzo na Ugani kukutana na wazalishajiwamayai, vifaranga, ng’ombe, kuku, mbuzi, kondoo, punda, nguruwe, viwanda vya nyama, ngozi na maziwa ili kujua mahitaji yao kwasasa ni yepi kwani waondio wataotengeneza ajenda za utafiti zenye uhitaji kwasasa.

Amekosoa mfumo wa uendeshaji wa tafiti za mifugo nchini kwakutokuwa na ajenda mahususi zinazohitajika kufanyiwa tafiti badala yake watafiti wengi wamekuwa wakiendesha tafiti za biashara kwa mataifa mengine ambazo hazina msaada kwa watanzania.

Amesema mfumo wakuibua ajenda za utafiti haufahamiki huku kukiwa na ushirikishwaji dhaifu wa wadau hali inayosababisha tafiti nyingi kushindwa kutoa majawabu ya matatizo katika sekta ya mifugo nchini huku matokeo na mazao yatafiti hizo yakiwafikia watu wachache kinyume na malengoyaSerikali.

Waziri Mpina alisema pamoja na kuwepo kwa njia zote hizo za uboreshaji Koosafu za mifugo bado kuna kasoro nyingi katika utaratibu unaotumika kuzalisha, kununua, kusambaza na kupandisha mifugo halii nayopelekea zoezi kuwa la kusuasua.

Alisema pamoja na mbegu hizo kuzalishwa na Serikali na kuuzwamrijammojakwash 3,000 lakini kutokana na kutokuwepo mfumo madhubuti wa usimamizi na kuachiwa wafanyabiashara binafsi kwenda kuwauzia wafugaji katiyash 20,000 hadish 60,000 kwa mrija jambo linawakatisha tamaa wafugaji na kutofikiwa malengo ya Serikali.

Hivyo Waziri Mpina alisema juhudi zote zinazofanywa na Serikali za kuzalisha mbegu bora katika vituo vyake vya NAIC Arusha na Taliri Mpwapwa haitakuwa na maana kama kasoro zilizopo sasa hazitaondolewa.

Kwa upande wake MkurungeziwaUtafiti, Mafunzo na UganiwaWizarayaMifugo na Uvuvi, Dk. Angello Mwila waalimhakikishia Waziri Mpina kuwa atasimamia kikamilifu utekelezaji wa maagizo yake ili kuhakikisha wafugaji wananufaika na jitihadahizozinazofanywa na Serikali ya awamu ya tano katika mkakati wake wauboreshaji wa koosafu ya mifugo nchini.

Naye Mkurungezi Mkuu wa TARILI, Dk. Eligy Shirima alisema mradi huo wa MOET unafadhili na COSTECH kwa gharama ya sh milioni 400 kwa ajili ya kununua vifaa vitakavyowezesha kukamua mbegu za dume na kuziweka kwenye jike maalum lililoandaliwa.

Dk Shirima alisema jike hilo baada ya kuwekewa hormones husaidia mayai mengi kuiva kwa maramoja na kurutubishwa ambapo mbegu zilizorutubishwa hunyonywa na kuhifadhiwa na kisha kusambazwa kwa wafugaji kwaajili ya uhamilishaji hatua ambayo itawezesha kupatika namifugo bora.


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.