Habari za Punde

Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Yaadhimishwa Kisiwani Pemba Uwanja wa Gombani leo.

Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akisalimiana na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Bi. Gadensia Kabaka, alipowasili katika viwanja vya Gombani Kisiwani Pemba kuhudhuria Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliofanyika Kitaifa Pemba kushoto Naibu Waziri wa Kazi Uwezeshaji Wazee Wanawake na Watoto Zanzibar Mhe. Shadya.na kulia Waziri wa Kazi Uwezeshaji Wazee Wanawake na Watoto Mhe. Maudline Castico.
MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akiongoza na Waziri wa Kazi Uwezashaji Wazee Wanawake na Watoto Zanzibar.Mhe. Maudline Castico, wakielekea katika eneo lililoandaliwa la maonesho ya Wajasiriamali Wanawake Kisiwani Pemba wakati wa hafla hiyo ya Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani ilioadhimishwa Kitaifa Kisiwani Pemba,leo 8-3-2019.
MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akiangalia Bidhaa za Wajasiriamali wa Kisiwani Pemba wakati akitembelea moanesho hayo katika viwanja vya Gombani Chakechake Pemba, kuadhimishi Siku ya Wanawake Duniani Kitaifa imefanyika Kisiwani Pemba leo.kushoto Mke wa Makamu wa Pili wa Zanzibar .Mama Asha Suleiman Iddi.
MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein na Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi, wakiangalia Bidhaa za Wajasiriamali Wanawake katika viwanja vya Gombani Chakechake Pemba, ikiwa ni Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, zilizofanyika Pemba Kitaifa leo. 
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akiwasalimiana Wanafunzi wa Madrasa walioandaliwa kwa ajili ya Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani zilizofanyika katika viwanja vya Gombani Chakechake Pemba leo.
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akiwasalimiana Wanawake wakati wa hafla ya Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani zilizofanyika Kitaifa Pemba katika Uwanja wa Gombani Chakechake Pemba leo.8-3-2019. 
Mke wa Rais wa Zanzibaer Mama Mwanamwema Shein, akihutubia wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani zilizofanyika katika Uwanja wa Gombani Chakechake Pemba, leo na kuhudhuriwa na Wanawake wa Mikoa Miwili ya Pemba.
Baadhi ya Wanawake Kisiwani Pemba wakifuatilia hutuba ya Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, wakati Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akihutubia hafla hiyo katika viwanja vya Gombani Chakechake Pemba leo.8-3-2019.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.