Waziri Mkuu mstaafu
Edward Lowassa akiwasili katika Ofisi ndogo za Chama cha Mapinduzi CCM Lumumba
jijini Dar es Salaam kabla ya kutangaza rasmi kurejea katika Chama cha
Mapinduzi CCM leo tarehe 1 Machi 2019.
Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa akisaini Kitabu cha
Wageni mara baada ya kuwasili katika Ofisi ndogo za Chama cha Mapinduzi CCM
Lumumba jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Dkt. John Pombe Magufuli
akishuhudia. Wakwanza kushoto ni Kada wa CCM Rostam Azizi
Mwenyekiti wa Chama cha
Mapinduzi CCM Rais Dkt. John Pombe
Magufuli akizungumza kabla ya kumkaribisha Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa
ambaye ametangaza kurejea chama cha Mapinduzi CCM akitokea chama cha CHADEMA
katika Ofisi ndogo za Chama cha Mapinduzi CCM Lumumba jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa akitangaza rasmi
kurejea chama cha Mapinduzi CCM mbele ya Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Dkt. John Pombe Magufuli, Makamu
Mwenyekiti wa CCM bara Philip Mangula, Katibu wa CCM Bashiru Ally, Waziri Mkuu
Kassim Majaliwa, pamojan na Kada wa CCM Rostam Azizi.
Mwenyekiti wa Chama cha
Mapinduzi CCM Rais Dkt. John Pombe
Magufuli akizungumza kumkaribisha Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa ambaye
amerejea rasmi CCM.
No comments:
Post a Comment