Habari za Punde

Kamati ya Rufaa Yairejesha Kalabu ya Ujamaa i

Na Hawa A  Ally -Zanzibar.
KAMATI ya Rufaa na Usuluhishi imeirejesha katika ligi ya sita bora klabu ya soka ya Ujamaa na kutupilia mbali maamuzi ya  Kamati ya mashindano na ligi ya ZFA Taifa .
Timu hiyo ambayo iliondoshwa katika hatua hiyo baada ya kubainika kwamba mchezo wao wa mwisho kati yao na White Bird walipanga matokeo kufatia ushindi wa mabao 11-0.
 Ujamaa baada ya kupewa hukumu hiyo  land a ngazi hadi katika kamati ya Rufaa na Usuluhishi ambayo ilitenguwa maamuzi hayo na kuirejesha.
Katika barua ya Kamati hiyo ilieleza ZFA ilishindwa kuithibitishia Kamati hiyo ni vitendo gani haswa ambavyo vilivyokuwa si vya kawaida vya utovu wa nidhamu hadi kufikia kufuta mchezo huo.
Barua hiyo iliyotiwa saini na Mwenyekiti wake Takky Abdulla Habibu na Katibu wake Suleiman Shaaban Fadhil ilisema kuwa katika maamuzi yao ZFA ilitegemea zaidi ripoti ya mwamuzi na kamishna wa mchezo ambazo Kamati imezikataa.
"Kamati imetenguwa maamuzi ya ZFA ya kuufuta mchezo na kuyabakisha matokeo Kama yalivyokuwa na ambae hakuridhika anaweza kwenda mahakama ya michezo Afrika CAS", alisema.
Barua hiyo ilifahamisha kwamba ZFA walikosea kanuni katika kufikia maamuzi kwa taarifa ambazo hazipo sahihi.
Aidha Takky kupitia barua hiyo walisema kuwa Kamati imesikitishwa sana na maamuzi yasiyozingatia Sheria na kanuni ya ZFA kwa kunukuu na kutoa maamuzi kwa vifungu ambavyo sio sahihi na bila ya kuwa na ushahidi wa kukitosheleza.
Barua hiyo ilieleza kuwa ZFA ilitumia kifungu cha 31 cha kanuni ya kendesha mashindano ambacho kinaelezea vitendo vyote vya utovu wa nidhamu vitakavyofanywa na timu, viongozi, wachezaji, wanachama, wapenzi, waamuzi na kamisaa ambavyo havikuelezwa katika kanuni hiyo.
Ujamaa  ilishuka dimbani Machi 18 mwaka huu, kucheza na White Bird iliibuka na ushindi wa mabao 11-0 wakati kabla ya mchezo huo ili iweze kufanikiwa kufuzu hatua hiyo ilikuwa ishinde mabao 9-0.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.