JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI
JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI
S. L. P. 1509,
DODOMA.
29 Aprili, 2019
|
|
Simu Nambari: +255-22-2113537
Telefax: + 255-22-2184569
Barua Pepe: fire.rescue@frf.go.tz
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
KAMISHNA
JENERALI WA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI NCHINI AFANYA MABADILIKO YA BAADHI YA
MAKAMANDA WA MIKOA
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto
na Uokoaji nchini, (CGF) Thobias Andengenye, amefanya mabadiliko ya baadhi ya
Makamanda wa Mikoa hapa nchini.
Makamanda walioguswa na mabadiliko hayo
ni Kamishna Msaidizi wa Zimamoto (ACF) Mohamed Kondo, aliyekuwa Kamanda wa
Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Kinondoni, anaenda kuwa Kamanda wa Zimamoto na
Uokoaji Mkoa wa Mbeya.
Kamishna Msaidizi (ACF) Juma Yange, aliyekuwa
Kitengo cha Utawala Mkoa wa Kinondoni, anakuwa Kamanda wa Zimamoto na Uokoaji
Mkoa wa Kizimamoto Kinondoni.
Mrakibu Msaidizi wa Zimamoto (ASF) John
Francis, aliyekuwa Chuo cha Zimamoto na Uokoaji Handeni Mkoani Tanga, anaenda
kuwa Kamanda wa Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Rukwa.
Vilevile, aliyekuwa Kamanda wa Zimamoto
na Uokoaji Mkoa wa Kigoma, Mrakibu Msaidizi wa Zimamoto (ASF) Athumani Basuka,
anaenda kuwa Kamanda wa Zimamoto na Uokoaji Wilaya ya Hai – Siha, nafasi yake
inachukuliwa na Mrakibu Msaidizi (ASF) Jumbe Juma.
Pia aliyekuwa Kamanda wa Kiwanja cha
Ndege Mkoa wa Iringa, Mkaguzi wa Zimamoto (INSP) Hamisi Dawa, anaenda kuwa
Kamanda wa Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Kagera.
Mabadiliko haya ni ya kawaida yanayotokea
ndani ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, katika kuongeza ufanisi wa utendaji
kazi.
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji linaendelea
kutoa wito kwa Wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa Makamanda wa Zimamoto
na Uokoaji Mikoa na Wilaya katika suala la Kinga na Tahadhari Dhidi ya majanga.
Imetolewa
na;
Joseph Mwasabeja
– (INSP)
Msemaji wa Jeshi
la Zimamoto na Uokoaji
Makao Makuu.
No comments:
Post a Comment