Habari za Punde

Mafunzo maalum kwa wafugaji nyuki yafanyika kisiwani Pemba

 BAADHI ya washiriki wa mafunzo ya ufugaji wa nyuki, ambao wataweza kuzalisha asali yenye viwango na itakayouzika ndani na nje ya Zanzibar, wakiwa katika mafunzo ya siku taatu yaliyoendeshwa na Taasisi ya Viwango Zanzibar (ZBS).(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
 MKURUGENZI mkuu wa Taasisi ya Viwango Zanzibar (ZBS) Khatib Mwadini Khatib, akizungumzia mikakati ya ZBS katika kuwafanya wafugaji wa nyuki kuweza kuzalisha asali bora na yenye viwango Nchini, mafunzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa kiwanda cha makonyo Wawi.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
 MWENYEKITI wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar na Mfugaji wa nyuki Maarufu katika jimbo la Mgogoni, Shehe Hamad Matar akizungumza katika kikao cha wafugaji wa nyuki Kisiwani Pemba, kilichoandaliwa na Taasisi ya Viwango Zanzibar, juu ya uzalishaji wa asali bora na yenye Viwango.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

 MKUU wa Mkoa wa Kusini Pemba Hemed Suleiman Abdalla, akifungua mafunzo ya siku tatu kwa wafugaji wa nyuki Kisiwani Pemba, mafunzo yalioandaliwa na Taasisi ya Viwango Zanzibar (ZBS), yaliyofanyika katika Kiwanda cha Makonyo Wawi.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.