Habari za Punde

Wanawake wa Iringa Wametakiwa Kugombea Nafasi Mbalimbali za Uongozi Katika Chaguzi za CCM Zijazo.

Mwenyekiti wa umoja wa wanawake wa chama cha mapinduzi (UWT) manispaa ya Iringa, Ashura Jongo akiongea na mwandishi wa habari wa blog hii katika mahojiano maalum yaliyofanyika katika viwanja halmashauri ya manispaa ya Iringa kuhusu wanawake wanaweza kuwa viongozi wazuri tatizo ni kushindwa kuthubutu.

Na.Fredy Mgunda - Iringa.
WANAWAKE manispaa ya Iringa wametakiwa kushiriki katika chaguzi mbalimbali zinazojitokeza hapa nchini ili kuongoza jamii inayowazunguka.
Akizungumza na blog hii mwenyekiti wa umoja wa wanawake wa chama cha mapinduzi (UWT) manispaa ya Iringa, Ashura Jongo alisema kuwa wanawake wanaweza kuwa viongozi wazuri tatizo ni kushindwa kuthubutu.
“Tangu mkutano wa beijing china umefanikisha kutujengea uwezo wananwake kwa kupata semina mbalimbali ambazo zimetusaidia kuwa viongozi wazuri wa kuweza kuongoza kwenye kila idara hivyo mkutano ule ulitusaidia sana wanawake” alisema Jongo
Jongo alisema kuwa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekuwa ikiwathamini wanawake kwa kuwapatia nafasi mbalimba za uongozi ambazo pia wanawake hao wamekuwa wakizitendea haki nafasi hizo.
“Nyinyi wenyewe mmekuwa mashaidi kuwa marais wetu wa awamu ya nne na serikali ya awamu ya tano mmeona jinsi gani viongozi wanawake wameongezaka katika nafasi mbalimbali za uongozi hasa kwenye nafasi za kuteuliwa na kuchaguliwa” alisema Jongo
Alisema kuwa ilikuwa vigumu mno kuona Rais akichagua viongozi wengi wanawake kama ilivyo hivi sasa ambavyo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli ameua mawaziri wengi wanawake,wakuu wa wilaya,wakuu wa mikoa pamoja na wakurugenzi kutoka sekta mbalimbali kwenye serikali ya awamu ya tano.
“Mmekuwa mashahidi mkiwaona viongozi wanawake walioteuliwa na waliogombea jinsi gani wanafanya kazi sawa sawa na wanaume hivyo wanawake tutaendelea kujiamini na kuongoza vizuri kati ngazi mbalimbali ambazo tutapata nafasi ya kuongoza” alisema Jongo
Aidha Jongo aliwataka wanawake kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi za uongozi kwa kuwa wanawake wamekuwa viongozi wazuri ila tatizo ni kushindwa kuthubutu.
“Saizi wanawake hawatakiwi kuwa na uoga wa kugombea mnatakiwa kukimbilia nafasi yeyote ili inayojitokeza kugombea kwa kuwa mnauwezo wa kuongoza na mmeonyesha kuwa mnaweza” alisema Jongo
Lakini Jongo aliwataka wanaume kuwapa nafasi wanawake kugombea nafasi mbalimbali na kuwaondolea uoga kwa kuwa wanaweza kuongoza katika nafasi nyeti za serikali.
Jongo  alimalizia kwa kusema kuwa wanawake wamekuwa viongozi hata kwenye familia ndio maana familia nyingi ambazo wanawake wamepewa nafasi wamekuwa viongozi wazuri wa familia.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.