Habari za Punde

Washindi wa Promosheni ya EzyPesa Kupitia Droo ya Pili ya Mwezi Wakabidhiwa Zawadi Zao

Mkuu wa Zantel Zanzibar,Bw.Mohamed Baucha (kushoto) akimkabidhi, Alhilal General Hemed,mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni moja,mmoja wa washindi kupitia droo ya pili ya mwezi ya promosheni ya  Zantel ya ‘Tumia EzyPesa Ushinde’katika hafla iliyofanyika Unguja.Wengine katika picha ni Maofisa wa kampuni hiyo,Meneja wa Bidhaa kitengo cha EzyPesa,Leonard Kameta (kushoto) na Meneja wa Chapa ya Zantel,David Maisori.
Mkuu wa Huduma na Bidhaa wa Zantel,Aneth Muga,akimkabidhi kitita cha fedha cha shilingi 500,000/-Mussa Mshenga ,mmoja wa washindi kupitia droo ya pili ya mwezi ya promosheni ya ‘Tumia EzyPesa Ushinde’ ya Zantel,katika hafla iliyofanyika Unguja.
Mkuu wa Huduma na Bidhaa wa Zantel, Aneth Muga,akimkabidhi kitita cha fedha,Muhammad Nasoro,mmoja wa washindi kupitia droo ya pili ya mwezi ya promosheni ya Tumia EzyPesa Ushinde ya Zantel,katika hafla iliyofanyika Unguja.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.