Katibu Mkuu Wizara ya
Maliasili na Utalii Prof.Adolf Mkenda (katikati) akizungumza na waandishi wa
habari (hawpo pichani) jana jijini Dodoma kuhusu namna ofisi yake imejipanga
kutumia jukwaa la mashindano ya AFCON U17 kutangaza fursa za utalii zilizopo
nchini katika kipindi cha mashindano hayo yatakayofanyika hivi karibuni nchini,
kutoka kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo
Bibi.Susan Mlawi na Kulia ni Katibu Mkuu Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF) Bw.Wilfred Kidao.
Katibu Mkuu Wizara ya
Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bibi.Susan Mlawi akitoa shukrani kwa
Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli kwa
kutoa fedha kiasi cha Bilioni Moja za
kuendesha mashindano ya AFCON U17 yatakayofanyika
hivi karibuni jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na waaandishi wa
habari (hawapo pichani) jana jijini Dodoma, Kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya
Maliasili na Utalii Prof.Adolf Mkenda.
Katibu Mkuu
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Bw.Wilfred Kidao (kulia)
akizungumza na waandishi wa habari
(hawapo pichani) jana jijini Dodoma kuhusu aina ya wageni wanaotarajiwa kufika
katika mashindano ya AFCON U17 yatakayofanyika nchini hivi karibuni ambapo
alieleza Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani Gianni Infantino
anatarajia kuja katika mashindano hayo, kushoto kwake ni Katibu Mkuu Wizara ya
Maliasili na Utalii Prof.Adolf Mkenda.
Na Anitha Jonas –
WHUSM.Dodoma.
Serikali ya dhamiria kutumia
jukwaa wa Mashindano ya AFCON U17 yatakayofanyika hivi karibuni kutangaza
vivutio vya utalii vilivyopo nchini ili kunufaika na wageni mbalimbali watakao
kuja kushiriki michuano hiyo ya Kimataifa.
Kauli hiyo imetolewa
jana na Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Prof.Adolf Mkenda wakati wa
kikao na Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo pamoja na viongozi
wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa lengo la kuhakiki mikakati
itakayotumika kutangaza vivutio hivyo ambavyo ni tunu ya Taifa.
“Sisi Wizara ya
Maliasili na Utalii tutahakikisha tunatumia jukwaa hili la michezo kuongeza
idadi ya watalii katika vivutio vya utalii nchini na tumejipanga vizuri kwa
matangazo mbalimbali ambayo yanamvuto wa ushawishi kwa watalii hawa wamichezo
kuvutiwa kufika katika maeneo hayo tunafukwe nzuri,Mbuga za wanyama,majengo ya
kale yenye hishoria mbalimbali,maporomoko ya maji na Mlima Kilimanjaro,”alisema
Prof.Mkenda.
Akiendelea kuzungumza
katika kikao hicho Prof.Mkenda alisisitiza kuwa ujio wa mashindano hayo ya
AFCON U17 nchini ni jambo lenye manufaa makubwa kwa taifa kwani kwa kujipanga
vizuri huu ndiyo wakati wa kunufaika kwa watanzania wote kupitia wageni hao,
wajasiriamali mbalimbali watanufaika kwa namna moja kwani wageni hao watahitaji
huduma mbalimbali kwa kipindi chote watakapo kuwa hapa nchini hivyo ni vyema
watanzania watumie fursa hii.
Kwa upande wa Katibu
Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bibi.Susan Mlawi alitoa
shukrani kwa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli kwa kutoa kiasi cha Shilingi Bilioni Moja kwa ajili ya kufanikisha
mashindano hayo tunashukuru sana kwani fedha hizo zitasaidia kukamilisha
uendeshaji wa shughuli mbalimbali katika kipindi cha mashindano.
“Wizara yangu kama mlezi wa Sekta ya Michezo
Nchi mpaka sasa tumesha kamilisha mambo
muhimu yote tuliyoagizwa CAF na vimebaki vitu vidogo sana ambavyo vitakamilika
ndani ya muda mfupi hivyo naweza kusema tupo tayari kwa mashindano,”alisema
Bibi.Mlawi.
Pamoja na hayo nae
Bibi.Mlawi alieleza kuwa mashindano hayo
yanataanza Aprili 14, Mwaka huu na Mechi ya ufunguzi inatarajiwa kufanyika
katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam hivyo ni vyema wakazi wa Jiji la
Dar es Salaam na kujipanga kwa ugeni huu na watanzania nivyema kujitokeza kwa
wingi kushuhudia tukio hili la kihistoria kwa taifa letu kuandaa mashindano
haya ya Kimataifa.
Halikadhalika nae
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira Tanzania (TFF) Bw.Wilfred Kidao alieleza
kuwa katika mashindano hayo Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani Gianni
Infantino atakuja hivyo ujio wake katika mashindano hayo utakuwa ni fursa ya
kutangaza nchi yetu, vilevile uongozi wote washirikisho la mpira wa Miguu
Afrika (CAF) nao utahamia Tanzania
katika kipindi chote cha mashindano.
“Katika mashindano
hayo ndipo wadau wa soka duniani wanakuja kusaka vijana wenye vipaji kwa ajili
ya kuwaunga katika timu zao kubwa za kimataifa mfano mchezaji kama Neymar ni
mmoja ya wachezaji waliyoibuliwa katika mashindano ya mpira kwa vijana chini ya
umri wa miaka 17 hivyo wapo wadau mbalimbali duniani watakuja kwa ajili ya
hilo,”alisema Kidao.
Wito kwa watanzania
ni kuwa tayari kwa ujio huu wa kimataifa na kujipanga vyema kunufaika na wageni
hawa kwa kuhakikisha wanakuwa watulivu na wakarimu kwa ajili ya kuiletea nchini
mafanikio katika uchumi.
No comments:
Post a Comment