Habari za Punde

Viongozi wa Serikali na Wananchi Wakihudhuria Hafla ya Dua Maalum ya Kuwaombea Mashujaa Yafanyika Migombani Zanzibar.

Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi akiongoza Viongozi wa Serikali ndugu na Jamaa katika Dua maalum ya kuwaombea Mashujaa ambapo imeanza kwa aliekuwa Rais wa Zanzibar  awamu ya Pili Sheikh Aboud Jumbe Mwinyi hadi kufikia kilele chake siku ya  07/04/2019 Kisiwandui Zanzibar,
Na Mwashungi Tahir-Maelezo Zanzibar      02 04.2019.
Mufti Mkuu wa Zanzibar Shekh Saleh Omar Kaabi amewaongoza Viongozi wa Serikali, Ndugu, Jamaa na Marafiki katika Dua maalum ya kuwaombea Viongozi mbali mbali wa Kitaifa waliotangulia mbele ya haki akiwemo Rais wa Awamu ya Pili wa Zanzibar Marehemu Aboud Jumbe Mwinyi.
Dua hiyo ilianza kwa kisomo cha Khitma na kuzuru Kaburi lake huko nyumbani kwa Marehem Migombani nje kidogo ya mji wa Zanzibar.
Akitoa nasaha zake Mufti Kaabi amesema Marehem Aboud Jumbe alikuwa ni Mtu aliyependa mashirikiano katika kuliongoza Taifa kwa umahiri.
Amesema Marehem pia alikuwa kiongozi muadilifu, aliyependa Wananchi wa Zanzibar washiriki kikamilifu katika kutafuta Elimu ndani na nje ya nchi ili kuendeleza maendeleo ya Zanzibar.
“Katika kupigania haki ya elimu kwa Wananchi Marehem alishajihisha wananchi kutafuta Nafasi za kusoma nje Skolaship na ndani ili kuhakikisha jamii inafaidika na fursa hizo” Alisema Shekh Kaabi
Katibu Mkuu wa Mufti sheikh Fadhil Soraga alisema iko haja kubwa ya kuwaombea dua viongozi kwani wamefanya mengi mazuri na yanaendelezwa hadi leo ikiwemo kushajihisha Wananchi kuishi kwa amani na utuluivu.
Amesema kuna umuhimu wa Viongozi waliopo madarakani kuyaendeleza kwa umakini mkubwa yote mazuri yaliyoasisiwa na viongozi hao kwa faida ya Kizazi cha sasa na baadae.
Awali Shekh Thabit Nooman Jongo kutoka Ofisi ya Mufti alisema lengo la dua hiyo ni kuwakumbuka viongozi wote walioshika nyadhifa mbali mbali za uongozi katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ambao kwa sasa wametangulia mbele ya haki ili Mwenyezi Mungu awasamehe makosa yao.
Alisema dhamira kubwa ya kuwaombea dua ni kuwakumbuka kwa yale waliyoyafanya katika nchi hii akiwemo Marehemu Rais Mstaafu Alhajj Aboud Jumbe Mwinyi  kwa mambo mengi yaliyoyafanyika katika uongozi wake.
Miongoni mwa mambo aliyoyafanya wakati wa uhai wake ni pamoja na kuwaunganisha wananchi wote wa Unguja na Pemba na kuwa kitu kimoja ili kuendelea kuishi kwa amani na utulivu kama alivyotaka Marehemu Mzee Karume.
Ibada hiyo ya kuwaombe Dua Viongozi wa Kitaifa itaendelea katika maeneo tofauti ambapo itaendelea Chukwani kwa kumuombea marehemu Mzee Thabit Kombo, na kesho itasomwa Dua ya Marehemu Idrissa  Abdulwakil huko Makunduchi.
Kwa upande wa Pemba Viongozi ndugu na Jamaa wa Marehemu watakusanyika kumuombea Waziri kiongozi mstaafu na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt Omar Ali Juma huko kijijini kwao Wawi.
Dua hiyo itakuwa endelevu kila ikifika kumbu kumbu ya Mashujaa ambayo kilele chake hufanyika April saba Kisiwandui mjini Zanzibar

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.