Habari za Punde

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Balozi Seif Ali Iddi Azungumza na Ujumbe wa Makamanda wa Jeshi Kutoka Nchini India.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Makamanda wa Vikosi mbali mbali vya Ulinzi na Usalama Kutoka Nchini India hapo Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Makamanda wa Vikosi mbali mbali vya Ulinzi na Usalama Kutoka Nchini India hapo Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.
Baadhi ya Makamanda wa Vikosi vya India na wale wenyeji wao wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania { JWTZ} wakifuatilia maelezo ya Balozi Seif hayupo pichani wakati wa mazungumzo yao.



 
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar akipokea zawadi maalum kutoka kwa Makamanda wa Vikosi mbali mbali vya Ulinzi na Usalama Kutoka Nchini India.

Balozi Seif  akiwa katika picha ya pamoja na Makamanda wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama kutoka Nchini India mara baada ya kufanya mazungumzo nao Ofisini kwake Vuga.




Na.Othman Khamis.OMPR.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amekutana kwa mazungumzo ya Timu ya Makamanda wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama kutoka Chuo cha Kijeshi Nchini India.

Timu hiyo iliyoongozwa na Balozi Mdogo wa India aliyepo Zanzibar Bwana T.B Barual ipo Tanzania kujifunza mambo mbali mbali ikiwemo masuala ya Historia ya Uhuru wa Tanganyika na Ukombozi wa Zanzibar.

Katika mazungumzo yao yaliyofanyika katika Ukumbi wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Vuga Mjini Zanzibar Balozi Seif  aliushauri Uongozi wa Timu hiyo kuandaa utaratibu maalum wa kuwapatia Mafunzo ya muda mfupi ama mrefu Maafisa na Wapiganaji wa Vikosi Maalum vya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Alisema India na Tanzania ikiwemo Zanzibar kwa ujumla Zina historia  ndefu katika masuala ya Kisiasa, Uchumi, Utamaduni na Biashara ambayo kwa sasa upo umuhimu wa kuelekeza nguvu hizo katika masuala ya Ulinzi ili Amani iendelee kutawala ndani ya Ukanda wa Bahari ya Hindi.

Nao kwa upande wao Makamanda hao kutoka Chuo cha Kijeshi cha India wameelezea faraja yao kutokana na mapokezi mazuri waliyoyapata ndani ya Vikosi vya Ulinzi vya Tanzania pamoja na Wananchi wenyewe kwa ujumla.

Walisema ukarimu walioupata Tanzania na Visiwa vya Zanzibar kwa ujumla umewapa matumaini makubwa ya kuwa na fikra na muelekeo wa kuitambelea tena Tanzania katika kipindi chengine kijacho.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.