Habari za Punde

Sera ya Michezo Kuondoa Changamoto za Timu NdogoNdogo Zanzibar.

Na, Hawa Ally, ZANZIBAR
NAIBU Waziri wa Vijana,Utamaduni, Sanaa na Michezo   Zanzibar  Lulu Msham Abdallah amesema Serikali kupitia Sera ya michezo  imeweka mikakati mbalimbali itakayosaidia kutatua changamoto zinazozikabili timu ndogo ndogo Nchini.
Amesema Mikakati hiyo inalengo la kuinua michezo wa mpira wa mguu Zanzibar kupitia timu ndogo ziweze kufanya vizuri.
Kauli hiyo ameitoa katika kikao cha Baraza la wawakilishi Chukwani Nje, Kidogo ya Mji wa Zanzibar wakati akijibu swali la Mwakilishi wa Jimbo la Chake chake Pemba (CCM) Suleiman Sarahani Said,
Alietaka kujua Mpango wa Serikali katika kutatua changamoto mbalimbali zinazozikabili timu ndogo ndogo ili ziweze kufanya vizuri.
Akijibu swali la Mwakilishi huyo Naibu Waziri alisema Serikali tayari imeshaanda Sera ya michezo ambapo ndani yake kuna mikakati mbalimbali itakayosaidia kutatua changamoto za Timu ndogo ndogo na kuweza kufanya vyema.
“Tumeshaandaa sera ya michezo ambayo kuna mikakati kadha ya kutatua changamoto zinazozikabili tumi zetu ndogondogo ili na wao wafanye vizuri”alieleza Naibu waziri huyo.
Aidha alieleza kuwa moja ya Mikakati ambayo imebeinisshwa katika Sera hiyo ni suala la udhamini na ufadhili katika michezo ili kutatua changamoto za vilabu.
Katika hatua nyingine Naibu waziri huyo akijibu swali la nyongeza la mwakilishi huyo alietaka kujua Serikali inachukua hatua gani katika kuhakikisha timu zinapewa ulinzi na usimamizi mzuri katika mchezo.
Naibu waziri kuwa Serikali kupitia Shirikisho la Mpira wa Miguu Zanzibar ZFF imeunda kamati Maalum ya kusimamia mashindano ya mpira wa miguu Zanzibar.
“kamati hii imepewa jukumu la kupanga ratiba,Waamuzi,viwanja na walinzi katika ligi zote zinazofanyika”alieleza Naibu Waziri huyo.
Aidha alieleza kuwa ili kuhakikisha suala la ulinzi mchezoni ZFF inakuwa inapeleka taarifa katika vituo vya polisi kwa ajili ya kupatiwa ulinzi panokuwa na mechi mbalimbali.
Katika maelezo yake alieleza kuwa Jeshi la Polisi Zanzibar limekuwa likikaa vikao mbalimbali na wadau wa soko na kukemea baadhi ya vitendo vya udhalilishaji mchezoni.
“Hivi karibuni kamishna wa alikutana na wadau wa michezo katika mkutano wa kujadili suala la udhalilishaji viwanjani ikiwemo kupigwa kwa waamuzi”alisema Naibu waziri

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.