Habari za Punde

Mgombe wa Nafasi ya Urais Shirikisho la Soka Zanzibar ZFF Ame Abdalla Ataja Sera Zake Indapo Atachagulia.

Na Hawa Ally, ZANZIBAR
Mgombea Urais wa Shirikisho la Soka Zanzibar ZFF Ame Abdalla Dunia ametaja vipaumbele nane endapo  atachagliwa kuwa Rais wa Shirikisho hilo ikiwemo Swala la nidhamu katika soka. 

Aliyasema hayo mbele ya waandishi wa habari katika kampeni za kuelekea uchaguzi wa Shirikisho hilo unaotarajia kufanyika June 2 mwaka huu. 

Alisema ili kuwe na soka la nidhamu na lenye mafanikio lazima kuwa na viongozi bora ambao watafata sheria, kanuni na katiba ya Shirikisho hilo.

Alisema uongozi wake hautakuwa wa mazoea badala yake utakuwa ni wakufuata misingi ya sheria na katiba ili kufikia malengo yaliyokusudiwa. 

Pia alisema kipaumbele cha pili atahakikisha anasimama vyema ligi ya Vijana kwa ngazi ya mikoa yote hususani ya vijijini ambayo ligi hiyo inasuasua ikilinganishwa na mikoa ya mjini.

Alisema Sambamba na hilo kipaumbele cha tatu atahakikisha kuwepo na mkurugenzi la benchi la ufundi katika mkoa ili kuzitengeneza

Aidha alisema kipaumbele uongozi wake utahakikisha unaboresha mashirikiano na waamuzi ikiwemo kuwepo kwa mikakati ya kuwapunguzi majukumu mengi kwa kuwepo waamuzi  watakaochezeha ligi kuu na kanda, Wilaya pamoja na mikoa. 

Alisema pia kipaumbele kingine cha tano ni kuwepo kwa Mafunzo maalum ya viongozi wa vilabu pamoja na makocha ili kuwajengea uwezo zaidi katika utendaji kazi zao. 

Aidha alisema kipaumbele muhimu kabisa katika kukuza soka la Zanzibar ni Swala zima la kutafuta udhamini wa ligi kuu ili kurejesha ushindani wa timu kama ilivyokuwa katika miaka ya nyuma. 

Alisema timu nyingi hazina uwezo hali inayopelekea hata kufikia hatua ya kutosajili wa chezaji wazuri kutokana na majukumu waliyonavyo hivyo Swala la udhamini katika soka la Zanzibar ataliangalia zaidi

Aidha alisema atahakikisha anasimamia na kudhibiti vitendo vya Rushwa ambavyo vimewkwa vikilalamikiwa na wadau wa soka ikiwemo timu zenyewe kupanga matokeo katika michezo ya mwisho jambo ambalo linapelekea kupanda daraja timu ambazo hazina uwezo kiuchezaji. 



Hata hivyo Alitaja kipaumbele kingine ni kuboresha mashirikiano ya kidiplomasia na mashirikisho mengine ikiwemo CAF, CECAFA pamoja FIFA ili soka la Zanzibar liweze kwenda na wakati kama ilivyo kwengine Duniani. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.