Habari za Punde

Wananchi Kisiwani Pemba Wapata Elimu ya Kuwajengea Uwezo Watendaji na Wawazeshaji wa Tasaf Kisiwani Pemba.

Ofisa Mdhamini Ofisi ya Makamo wa pili wa  Rais Pemba, Ali Salim Mata, akitowa maelezo juu ya lengo la kuwepo mkutano wa kuwajengea uwezo Watendaji na Wawezeshaji wa Tasaf Pemba, huko katika Ukumbi wa Tasaf Pemba.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa maendeleo ya Jamii Tanzania (TASAF) ,Ladislaus Mwamanga , akifunguwa kikao cha kuwajengea Uwezo Watendaji wa mfuko huo Kisiwani Pemba iliofanyika katika ukumbi wa Tasaf Pemba.
Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba, ambae pia ni Mwenyekiti wa kamati ya Uongozi ya Tasaf Kisiwani humo, Hemed Suleiman Abdalla, akitowa salamu a Kamati ya Uongozi ya mfuko huo kwa Mkurugenzi mtendaji wa Tasaf Tanzania , Ladislaus Mwamanga , mara baada ya kufunguwa kikao cha kuwajengea uwezo Watendaji wa Tasaf huko katika Ukumbi wa Tasaf Pemba.
Baadhi ya Wawezeshaji wa mfuko wa maendeleo ya Jamii Tasaf Pemba, wakiwa katika kikao cha kuwajengea uwezo ili waweze kusimamia vyema majukumu yao.

Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba ba Kaskazini  na Mkurugenzi Mtendaji wa Tasaf Tanzania,
Ladislaus Mwamanga na Watendaji na Wawezeshaji wa Mfuko wa Tasaf Kisiwani Pemba wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumaliza mkutano huo uliofanyika katika jengo la Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Pemba.
Picha na Bakari  Mussa -Pemba.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.