Katibu wa Hamasa na Chipukizi Jumuiya ya Vijana ya Chama cha Mapinduzi
(UVCCM) Mkoa wa Tanga Waziri Mohamed
VIJANA mkoani Tanga wametakiwa kujitokeza kwa wingi kuwania nafasi
mbalimbali kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka huu na ule wa
wabunge na madiwani mwakani.
Wito huo ulitolewa leo na Katibu wa Hamasa na Chipukizi Jumuiya ya
Vijana ya Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Tanga Waziri Mohamed
wakati akizungumza na waandishi wa habari.
Alisema lazima vijana waweze kuona umuhimu wa kujikita kwenye nafasi
mbalimbali za uongozi ili kuweza kuwatumikia wananchi kwa uadilifu na
uzalendo mkubwa .
“Kama Rais alivyofanya kuwaamini vijana kwenye teuzi mbalimbali hivyo
nasi tujitokeze kwa wingi kwenye uchaguzi huo kuomba kugombea nafasi
mbalimbali na tunaweza kupata fursa na kuweza kuwatumikia wananchi
“Alisema .
Hata hivyo alisema wao kama Jumuiya ya Vijana watawahamasisha vijana
ambao wanadhani wanasifa za kuwania nafasi hizo ili waweze
kuchangamkia fursa hiyo muhimu kwa jamii.
Katika hatua nyengine Katibu huyo ametumia milioni 10 kwa ajili ya
ujenzi wa ofisi ya CCM kata ya Mlingano wilayani Muheza.
Alisema aliamua kufanya ujenzi huo baada ya kata hiyo haina
ofisi kwa kipindi kirefu na kulazimika kutumia maeneo mengine
na hivyo ndipo alipoamua kufanikisha ofisi hiyo.
“Baada ya kuchaguliwa kuwa Katibu Mwenezi wa CCM Kata hiyo na baadae
kuchaguliwa kuwa Katibu wa Hamasa na Chipukizi Jumuiya ya Vijana ya
Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Tanga ndipo nilipoanza ujenzi huo.
No comments:
Post a Comment