Habari za Punde

WAKULIMA WA ALIZETI WALIA NA MASHARTI YA MIKOPO KATIKA TAASISI ZA FEDHA

Kaimu katibu tawala anayeshughulikia masuala ya Kilimo,Uchumi na uwezeshaji mkoa wa Songwe ,Evance Kakulanga akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kongamano la siku tatu kwa wadau wa zao la Alizeti liliofanyika mkaoni Mbeya.
Mkurugenzi Mtendaji wa  Programu ya kuendeleza Mifumo ya Masoko ya Kilimo Tanzania (AMDT) Michael Kirumba akizungumza wakati wa Kongamano hilo la siku tatu .
Baadhi ya washiriki wakifuatili mada zilizokuwa zikitolewa katika Kongamano hilo.
Baadhi ya Washiriki wa Kongamano hilo wakichangia mada wakati wa mijadala katika Kongamano hilo.
Washiriki wa kongamano la mafunzo lililoandaliwa na Programu ya kuendeleza Mifumo ya Masoko ya Kilimo Tanzania (AMDT) wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kongmano hilo lililofanyika mkoani Mbeya.

Na  Dixon Busagaga wa Michuzi TV .
MASHARTI ya mikopo yanayotolewa na taasisi za fedha nchini kwa ajili ya wakulima yanatajwa kuwa kikwazo kwa baadhi ya wakulima wa zao la Alizeti nchini kushindwa kufanya kilimo chenye tija kwa zao hilo.

Moja ya Masharti hayo ni pamoja na wakulima kujiunga katika vikundi ili kurahisisha upatikanaji wa mikopo jambo ambalo wakulima wengi wa Alizeti wameshindwa kutumiza sharti hilo kutokana na kuamua kufanya shughuli za kilimo bila ya kuwa kwenye kikundi.

Kutokana na hali hiyo tayari Wakulima wa zao la Alizeti nchini wameshauriwa kujiunga katika vikundi ikiwa ni pamoja na kuanzisha vyama vya ushirika ambavyo vitasaidia katika kuanzisha mchakato wa kupata mikopo pamoja na pembejeo za kilimo kwa ajili ya zao hilo.

Ushauri huo umetolewa wakati wa Kongamano la mafunzo liloandaliwa na Taasisi ya Kuendeleza Mifumo ya Masoko ya Kilimo Tanzanina (AMDT),kongamano lililofanyika mkoani Mbeya likiwahusisha wadau mbalimbali wa zao la Alizeti kutoka mikoa 16 ya Tanzania bara.

Wakati wa mijadala katika kongamano hilo baadhi ya wakulima na wadau wa zao la Alizeti walisema kumekuwepo na changamoto ya upatikanaji wa mikopo kwa wakulima, hali ambayo wameitaja kuwa ni kikwazo katika kumsaidia mkulima mdogo wa zao hilo.

“Ni ukweli usiopingika wengi wetu licha ya kuvutiwa na kilimo cha Alizeti, kutokana na hamasa na elimu ambayo tumekuwa tukiipata kutoka kwa wadau wetu wa kilimo lakini tunashindwa kufanya kilimo chenye tija kutokana na uwezo wetu kuwa mdogo” alisema Anita Mwakyoma ambaye ni msindikaji wa mafuta ya Alizeti.

Alisema pamoja na ugumu wa upatikanaji wa mikopo, bado wakulima wengi wameshindwa kumudu bei za mbegu bora za Alizeti zinazopatikana sokoni na hivyo kulazimika kutumia mbegu zisizokuwa na ubora ambazo zimekuwa hazitoi mbegu za kutosha hali ambayo inayomfanya mkulima asinufaike na kilimo.

“Pamekuwepo na jitihada kubwa sana inayofanya na wadau wa kilimo na hasa maafisa ugani katika kutuhamasisha juu ya umuhimu wa matumizi ya mbegu bora ambazo hutoa mazao mengi wakati wa mavuno, lakini kutokana na gharama kubwa ya mbegu hizi wengi wetu tunashindwa.”alisema Mwakyoma.

Naye Mkulima wa Alizeti katika mkoa wa Songwe Sophia Mwanandenga aliziomba mamlaka zinazohusika na Kilimo hususani upande wa Pembejeo kuangalia namna zitakavyomsaidia mkulima kupata mbegu bora kwa bei nafuu.


Akijibu hoja ya upatikanaji wa mikopo kwa wakulima wadogo, mwakilishi wa Benki ya Posta Nchini Tawi la Mbeya,Leonard Katamba alisema kwa muda mrefu mkulima mdogo  amekuwa hakopesheki kutokana na kushindwa kufikia vigezo vilivyowekwa na baadhi ya taasisi za fedha.

“Kwa kutambua mchango wa mkulima katika ukuaji wa uchumi nchini, TPB tumeanzisha mpango maalumu wa kuwahamasisha wakulima kujiunga na vikundi, hatua ambayo itakuwa ni msaada kwa mkulima kuweza kupata mikopo pindi atakapokuwa anahitaji.”alisema Katamba.

“Kwa sasa tunawahamasisha wajiunge katika vikundi ili waweze kufikiwa kwa urahisi na wadau mbalimbali walioko katika mnyororo wa thamani wa zao la Alizeti , na tayari tumeanza kuyaona mafanikio katika maeneo ya Mpwapwa mkoani Dodoma, Iringa na Mkoa wa Njombe”aliongeza Katamba .

Alisema katika maeneo hayo tayari wakulima wamehamasishwa kuanzisha vikundi ambavyo hadi sasa licha ya kusubili mikopo kutoka benki tayari wameanza utamaduni wa kujiwekea akiba jambo ambalo linatajwa kma hatua njema.

“Hii kwetu ni hatua nzuri maana kwa kujiwekea akiba mkulima hata lazimika kuchukua mikopo bila sababu ya msingi maana tayari wanakuwa na akiba ambayo inaweza kuwasaidia katika hatua mbalimbali wakati wa kilimo.”alisema Katamba.

Kwa Upande wake mtafiti wa mbegu kutoka taasisi ya utafiti wa mbegu nchini (TARI) Samweli Mwenda alisema taasisi yao mpaka sasa inaendelea na tafiti mbalimbali ambazo zimelenga kumsaidia mkulima kupata mbegu bora na ambayo itakuwa na tija kwa mkulima wa Alizeti nchini.

“Sisi kama taasisi ya serikali jukumu letu ni kuhakikisha kuwa tunapata mbegu bora na zenye tija na mpaka sasa tunaendelea na tafiti mbalimbali ili kuleta mbegu mpya pamoja na kusafisha au kuboresha mbegu mbalimbali zilizopo sokoni ili mkulima aweze kupata mavuno mengi na yenye tija. alisema Mwenda.

Naye Meneja wa zao la Alizeti kutoka taasisi ya Taasisi ya Kuendeleza Mifumo ya Masoko ya Kilimo Tanzanina AMDT, Martin Mgallah amesema kuwa wao kama taasisi ambayo imekusudia kumuinua mkulima wa zao la Alizeti nchini itaendelea kwa kushirikiana na wadau wake kuhakikisha wakulima wanakuwa katika vikundi ili viweze kuwa na sifa ya kukopesheka hatua ambayo itakuwa ndio mkombozi kwa mkulima.

Taasisi ya Kuendeleza Mifumo ya Kimasoko Katika Kilimo Tanzania,AMDT imekuwa ikitekeleza miradi mbalimbali katika mikoa 15 nchi ambapo mpaka sasa zaidi ya wakulima 150,000 wamekwisha fikiwa kupitia mradi huu ambao lengo lake kubwa ni kumwezesha mkulima mdogo kupata tija katika kilimo hicho kwa kulima na kuzingatia kanuni bora za kilimo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.