Habari za Punde

WAZIRI UMMY AKABIDHI SHEHENA YA FUTARI KWA TAASISI NNE KUBWA ZA KIISLAMU JIJINI TANGA

MBUNGE wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) Ummy Mwalimu ambaye pia ni Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto kulia akimkabidhi sehemu ya shehena ya futari Katibu wa Taasisi ya Kiislamu ya Shamsi Maarifa ya Jijini Tanga Omari Athumani Futari hiyo kushoto ambapo vitu viliyotolewa kwa kila taasisi ni  Mchele kilo 100, Maharage kilo 100, Tambi mifuko miwili, Sukari kilo 25, Unga wa Ngano kilo 50, Unga wa Sembe kg 25, Mafuta ya kula lita 20 na majani ya chai ambazo walikabidhiwa
 MBUNGE wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) Ummy Mwalimu ambaye pia ni Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto kulia akimkabidhi sehemu ya shehena ya futari Katibu wa Taasisi ya Kiislamu ya Shamsi Maarifa ya Jijini Tanga Omari Athumani Futari kushoto ambapo vvitu viliyotolewa na Mchele kilo 100, Maharage kilo 100, Tambi mifuko miwili, Sukari kilo 25, Unga wa Ngano kilo 50, Unga wa Sembe kg 25, Mafuta ya kula lita 20 na majani ya chai ambazo walikabidhiwa

 MBUNGE wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) Ummy Mwalimu ambaye pia ni Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto kulia akimkabidhi sehemu ya shehena ya futari mmoja wa wanafunzi wa Taasisi ya Kiislamu ya Shamsi Maarifa Imamu Abdallah
 Sehemu ya Shehena ya futari ilivyotolewa na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) Ummy Mwalimu ambaye pia ni Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto kwa ajili ya Taasisi kubwa nne za Kiislamu Jijini Tanga
Sehemu ya Shehena ya Futari iliyotolewa na Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga(CCM) kwa Taasisi nne kubwa za Kiislamu Jijini Tanga

MBUNGE wa Viti Maalumu Mkoani Tanga (CCM) Ummy Mwalimu kushoto akimsikiliza Katibu wa Taasisi ya Kiislamu ya Shamsi Maarifa ya Jijini Tanga Omari Athumani kulia mara baada ya kufanya makabidhiano ya shehena ya futari 
MBUNGE wa Viti Maalumu Mkoani Tanga (CCM) Ummy Mwalimu ametoa shehena ya futari kwa Taasisi kubwa za nne za Kiislamu Jijini hapa kwa ajili ya matumizi kwenye mwezi mtukufu wa ramadhani
Taasisi ambazo zimepata futari hiyo iliyotolewa na Mbunge Ummy ambaye pia ni Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii  Jinsia Wazee na Watoto ni Shamsi Maarifa ,Zaharau,Maawal na Tamta ambapo halfa ya makabidhiano hayo yalifanywa na kwenye taasisi zao.
Futari iliyotolewa kwa kila taasisi ni Mchele kilo 100, Maharage kilo 100, Tambi mifuko miwili, Sukari kilo 25, Unga wa Ngano kilo 50, Unga wa Sembe kg 25, Mafuta ya kula lita 20 na majani ya chai ambazo walikabidhiwa
Akizungumza baada ya kukabidhi futari hiyo Waziri Ummy alisema ameona atoe futari hiyo kwa taasisi hizo kubwa kwa niaba ya wakazi wa mkoa wa Tanga akiwa kama kiongozi wa mkoa huo kwenye kipindi hiki cha mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.
“Nikiwa kama mwana jamii na kiongozi wa mkoa wa Tanga nimeona nitoe futari kwa taasisi hizo kubwa nne kwa niaba ya wakazi wa Tanga ambazo zinafundisha vijana wetu kutoka maeneo mbalimbali elimu ya dini na mambo yanayohimizwa kwenye dini kwani shamsi maarifa ina wanafunzi 600,zaharau wanafunzi 200“Alisema.
Aidha pia aliwataka waislamu mkoani Tanga kuendelea kutenda mambo mema kwenye mwezi mtukufu wa ramadahani na kuendelea kuyatenda hata baada ya kumalizika mwezi huo ikiwemo kufanya ibada kila wakati.
Awali akizungumza mara baada ya makabidhiano hayo Katibu wa Taasisi ya Kiislamu ya Shamsi Maarifa iliyopo Duga Jijini humo Omari Athumani alimshukuru Waziri Ummy huku wakieleza wamepata mtu wa pekee Tanga kutokana na kuwa karibu na wananchi kila wakati kwa kutoa misaada.
Alisema kwamba hii sio mara ya kwanza kutokana na kwamba amekuwa akiwajali wananchi kwa kujitolea vitu mbalimbali wakati wa mwezi mtukufu wa ramadani na hivyo ni wazi kwamba tumepata mtu wetu sahihi kwa mkoa wa Tanga.
“Tuna mshukuru Mwenyezi Mungu akuongoze kwenye kazi zako na aendelee kukupa afya njema wewe a kubwa wataendelea kuliombea Taifa Amani na kumuombea Afya njema Rais wetu Dkt John Magufuli na kumtakia mafanikio katika kuliongoza Taifa”Alisema

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.