Habari za Punde

Kikosi cha KMKM Chajiandaa Michuano ya Kagame Cup.

Na.Mwanajuma. Juma.
WAWAKILISHI wa Zanzibar kwenye michuano ya Kombe la Kagame timu ya KMKM wamejipanga vyema kuhakikisha wanafanya vizuri kwenye michuano hiyo.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi Kocha wa timu hiyo Ame Msimu amesema mashindano hayo  ni makubwa kwa Afrika mashariki ila kwa upande wao wamejipanga ili kuweza kuyakabili.

"Niseme  tu ndugu mwandishi mashindano haya ni makubwa na si kwetu tu bali kwa Afrika mashariki lakini tumejipanga ili kuona kwa kiasi kikubwa tunakabiliana nayo", alisema.

Alisema kuwa tayari Kikosi chake kimeanza mazoezi ya utimamu wa mwili kwa kufanya mazoezi pwani.

Alisema mazoezi hayo kwa kuanzia yamewashirikisha wachezaji wote waliopo Zanzibar na wale ambao wapo bara wakati wowote wataungana na wenzao .

"Tuna kama siku ya tatu tokea tuanze mazoezi na tunao wachezaji wanaoishi Zanzibar kwa wale wa  Tanzania bara watawasili muda wowote kuanzis sasa", alisema.

Hata hivyo alisema kuwa mazoezi hayo hayalengi kwa ajili ya kagame tu, bali ni kwa ajili pia ya maandalizi kwa Msimu wa ligi kuu ya Zanzibar 2019/2020.

KMKM ndio mabingwa wa Zanzibar ambao waliukosa ubingwa huo kwa miaka minne mfululizo tokea 2014/2015 wakati ambao ligi hiyo ilikuwa ikidhaminiwa na Grand Malt.

UONGOZI wa timu ya soka ya Mafunzo umesema kuwa bado haujaanza kufanya usajili wa aina yoyote ya wachezaji ingawa lengo lao ni kusajili wachezaji wanne.

Katibu wa michezo na Utamaduni wa Chuo Cha Mafunzo Zanzibar Makame Fadau Makame alisema kuwa katika usajili wao wanatarajia kumsajili mlinda mlango, walinzi wawili na mshambuliaji mmoja.

"Hatujasajili bado lakini matarajio yetu kusajili wachezaji wanne", alisema.

Alifahamisha kwamba tayari uongozi wao wameshaanza mazungumzo na wachezaji ambao watawasajili ingawa alisema hayuko tayari kuwataja.

Alieleza kuwa wachezaji hao wanaendelea nao vyema na mazungumzo na kuna matumaini makubwa ya kuweza kuwapata.

"Tunaendelea nao vizuri na mazungumzo na wanaonesha matumaini sikutajii nani na nani mpaka pale muda wa uhamisho na usajili utakapowadia", alisema.


Zoezi la usajili na uhamisho awali lilitangazwa kuanza Juni mosi mwaka huu, lakini limesitishwa baada ya kupatikana viongozi wapya wa Shirikisho la Soka Zanzibar ZFF.

KAMATI ya kusimamia mashindano ya kombe la Hassan Gharib CUP kimetoa makundi ya timu zitakazoshiriki michuano hiyo inayotarajiwa kuanza Juni 22 mwaka huu.

Michuano hiyo ambayo inashirikisha timu 16 zimepangwa makundi manne ambapo Kila kundi litakuwa.na timu nne.

Kwa mujibu wa Mratibu wa mashindano hayo Talib Haji Khamis ametaja kundi A litakuwa.na timu za  Mitondooni Boys,  Qttar FC, Machinjira Cemp na  Njugu mawe.

Kundi  B linaundwa na Mtunda Maraha, Kwerekwe City,  Kane Combain na Dimani Star wakati.kundi FC Worrious, Pangawe FC,  Kisaka saka na Wabunge FC.

Kwa.upande wa timu zinazounda kundi D. Time Shela, Rong Ton,  Dunga.(12) na  Bati Jekundu.

Khamis alisema kuwa  Ratiba kamili ya michuano hiyo  itatolewa kesho Juni 15 mwaka huu,  saa10 jioni huku timu kutoka kundi A ndizo zitakazofunguwa dimba ingawa hazikutajwa ni timu gani na gani.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.