Habari za Punde

Waziri Castico aiasa jamii kuwashirikisha watoto kuweza kujikinga na vitendo vya udhalilishaji

NA MWAJUMA JUMA
WAZIRI wa Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Wanawake naWatoto Moudline Castico ameitaka jamii kuwashirikisha watoto ili kuweza kujuwa kujikinga na vitendo vya udhalilishaji.

Wito huo aliutoa mwishoni mwa wiki iliyo katika Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika iliyofanyika kwenye viwanja vya SOS Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, ambayo imeandaliwa kwa pamoja na SOS,  C-Sema, Save The Children, Action Aid Tanzania, Path Finder International, ZAFELA, TAMWA pamoja na Serikali waliandaa tamasha maalumu la michezo lililowashirikisha watoto wa 600 kutoka shule mbali mbali.

Alisema kuwa ushirikishwaji wa watoto ni moja kati ya haki ya msingi za watoto ambazo huwa na upeo mpana wa kuweza kutambuwa yaliyopo mbele yao na kuweza kukabiliana nayo.

Alieleza kuwa siku hiyo ya Mtoto wa Afrika inatoa fursa ya kupima utekelezaji wa haki za watoto na msukumo baina ya watoto na jamii.

“Haki ya mtoto si kumpa mahitaji tu ya msingi bali pia unapaswa kama mzazi ukae nae, uzungumze nae ili ujuwe tatizo linalomsibu na kuweza kulitatuwa”, alisema.

Mapema Mkurugenzi wa Wazee na Ustawi wa Jamii, Wahida Maabadi alisema kuwa watoto nao wanajukumu la kuhakikisha wanapinga vitendo vya udhalilishaji wanavyofanyiwa .

Alisema kuwa watoto wa Afrika Kusini ambao ndio chimbuko la siku hii, waliweza kupaza sauti zao kupinga ubaguzi lakini wao Zanzibar na Tanzania kwa ujumla wanatakiwa wapinge vitendo vya udhalilishaji ambavyo zimekithiri.

Mjumbe wa Bodi ya SOS, Nassor Dachi alisema kuwa ukatili dhidi ya watoto utaweza kumalizika iwapo vyombo vya sheria vitakuwa tayari kuwa kitu kimoja kufanya kazi kwa mashirikiano.

Alisema kuwa vyombo hivyo vikiwajibika ipasavyo kwa hakika vitendo hivyo vitapunguwa au kupotea kabisa na kuwataka watoto wasisite kutoa taarifa iwapo kutakuwa na viashiria vya kufanyiwa udhalilishaji kwa mtu anaemjua na hata asiemjua

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.