Habari za Punde

CCM M/Magharibi waja na utaratibu mpya wa vikao vya kichama matawini

NA MWAJUMA JUMA
CHAMA Cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja kimeanzisha utaratibu mpya wa ufanyaji wa vikao matawini kwa wanachama wake kwa kuwakutanisha kwa pamoja na kuwapa mafunzo.

Mafunzo hayo ya siku moja yalifanyika mwisho wa wiki iliyopita ambayo yanalenga kuweza kuona kasoro zilizopo ndani ya matawi na kuweza kuzifanyia marekebisho.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufunguwa mafunzo hayo Mwenyekiti wa Mkoa huo Talib Ali Talib alisema kuwa mkoa wao una matawi 59 ambayo yote kwa pamoja wamewaita viongozi wao na kufanya vikao vya kawaida pamoja na kuwapatia mafunzo ambayo yatawasaidia katika utekelezaji wa kazi zao.

Alisema kuwa hii yote ni safari ya 2020 ili waweze kufanya vizuri katika uchaguzi kwani wanaamini kwamba matawi yanapokuwa vizuri ndio msingi mzuri wa chama.

“Tunaamini kwamba matawi ndo kila kitu na kuharinbika kwa matawi ndio kuharibika kwa chama kizima hivyo kwa kuona umuhimu huo tumeona tuwakutanishe na kuwapa mafunzo zaidi ili kujipanga kwa ajili ya mwaka 2020”, alisema.

Alieleza kuwa kwa muda huu uliobakia hakuna kulala ni kuweka mikakati imara ili waweze kufanya vizuri na kushinda majimbo yote tisa yaliyomo kwenye mkoa wao.

Alieleza lengo hasa la kuwakutanisha viongozi wa matawi hayo kufanya vikao vya pamoja ni  baada ya kugunduwa kwamba ndani ya vikao hivyo kuna viongozi wakongwe na vijana hivyo wamemauwa kuwakutanisha ili kukazia usawa wao katika kutekeleza majukumu yao.

Aidha alisema kuwa hatua hiyo pia inalenga kuendana na agizo la viongozi wakuu wa chama wa kuwataka watu kutofanya kazi kwa mazoea na wajuwe kwamba wanafanyakazi ndani ya chama na sio kama hawawaamini.

“Hali ya kisiasa ndani ya matawi ndio inayojenga chama tupo kwa ajili ya kuangalia ambapo baada ya kujuwa hali ilivyo huko tutajuwa ipo kw akiasi gani na vipi tunayafanyia kazi”, alisema.

Mapema Kaimu Katibu Mkuu wa CCM Mkoa huo Mwinyi Hassana alisema kuwa leo lao ni kufanya vikao vya kawaida vya kamati ya siasa ambayo kwa mujibu wa katiba hufanyika kila baada ya miezi mitatu.

Alisema kuwa mbali na kuwa ni suala la kikatiba lakini  pia wamegunduwa ndani ya matawi hawafanyi vizuri hivyo wamewaita ili kuona jinsi wanavyotekeleza wajibu wao na kama kuna tatizo waweze kuwarekebisha, hivyo kikao hicho ndani yake kina mafunzo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.