Habari za Punde

ZFF kutoa mafunzo kwa makocha wa makipa


Na Hawa Ally,

SHIRIKISHO la soka Zanzibar ZFF  linatarajia kutoa mafunzo ya siku saba  kwa makocha wa makipa Ili kuwajengea uwezo pamoja na kuwa na vyeti kisheria. 

Mafunzo hayo yanatarajiiwa kufanyika mapema July mosi mwaka huu katika ukumbi wa Uwanja wa Amaan kisiwani Unguja huku mkufunzi wa mafunzo hayo anatarajiwa kuwa Kocha Salehe Ahmed Machupa akishilikiana na Kocha kutoka Tanzania bara ambae bado yupo katika mazungumzo ya mwisho. 

Akizungumza na Waandishi wa habari Afisa habari wa shirikisho hilo Adam Natepe alisema makocha wote ambao hawana vyeti wanatakiwa kuhudhulia mafunzo hayo Ili kufata sheria ya CAFna FIFA kwa makocha kuwa na vyeti na leseni Ili waweze kuendesha shughuli zao. 

Alisema ZFF inawataka makocha hao kumtumia fursa hii ili makocha ambao hawana vyeti waweze kupata vyeti hivyo kabla ya kuanza kwa msimu wa ligi ambao inatarajiwa kuanza August mwaka huu. 

"Tunawaomba makocha ambao hawana vyeti waje katika kozi hii muhimu kwao wao pamoja na kuzisaidia timu Ili mwisho wa siku  wanaweza hata kupata ajira katika vilabu vingine vya nje ya Zanzibar." Alisema 

Aidha alisema shirikisho la Soka linawaatarifu makocha wote wa makipa ambao hawana vyeti hawataruhusiwa kukaa katika benchi la ufundi kwani kufanya hivyo ni kinyume cha sheria ya CAF. 

Alisema Kocha yoyote ambae atafanya hivyo atachukuliwa hatua za kisheria ikiwemo klabu kulipa faini ya shilingi laki tano. 



"ZFF haitamuonea huruma Kocha yoyote ambae hana cheti halafu akawekwa katika benchi la ufundi, litakuwa makini na wakali katika swala hili na halitasita kuwachukulia hatua" Alisema. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.