Habari za Punde

Veterani wa KMKM na Zimamoto watinga fainali bonanza la KMKM

NA MWAJUMA JUMA
MAAFANDE wa timu za soka za Veteran za KMKM na Zimamoto wamefanikiwa kutinga hatua ya fainali ya bonanza la KMKM linalotarajiwa kufikia kilele chake Jumapili .

Timu hizo zote mbili zilifikia hatua hiyo baada ya juzi kushinda katika mechi zao za nusu fainali zilizochezwa katika viwanja viwili tofauti.

KMKM ambao ndio wenyeji wa bonanza hilo lililoandaliwa na KMKM Klabu ilishuka katika dimba la Ziwani Bomani na kufanikiwa kuifunga JKU mabao 2-0 wakati Zimamoto ilicheza kwenye uwanja wa Kikwwajuni na kutoka na ushindi wa penant 5-4 kufatia dakika 90 kutoka sare ya kutokufungana.

KMKM katika mchezo wake huo ilifanikiwa kuibuka na ushindi huo kupitia kwa wachezaji wake Hashim Ramadhan dakika ya 36 na Juma Faki Mbwana dakika ya 60.

Jumla ya timu nane zilikuwa zinashiriki bonanza hilo ambalo lina lengo la kujitangaza kwa kikosi hicho kupitia michezo pamoja na kukabidhi vikombe vya ushndi kwa timu ya KMKM Veteran na KMKM Klabu ambavyo wamevipata kupitia mashindano ligi pamoja na Mei Day.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.